REA yamtakia Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan heri ya kuadhimisha siku ya kuzaliwa...Soma aliyoyasema Mheshimiwa Rais Samia hapa


"Samia ni mtoto wa tatu katika familia ya watoto 15, lakini mama wawili na ni mtoto aliyetoka kwenye Familia ya Baba Mwalimu na Mama wote wawili ni wamama wa nyumbani.

"Kuanzia Darasa la Awali mpaka nafika kidato cha nne nimesoma shule kama 10 hivi na hiyo ni kwa sababu Baba yangu alikuwa Mwalimu.Kwa hiyo alikuwa anahamishwa vituo vingi vingi vya kazi, kwa hiyo kila anapohamishwa na mimi niko nyuma.

"Nikiwa na miaka minane...tisa hivi niliishi na Dada yangu na yeye alikuwa Muuguzi Mkunga nikaishi nae kwa miaka kadhaa kutoka hapo hadi nimekuwa mkubwa nilikuwa mikononi mwake, nimezunguka sana ukienda Pemba na Unguja nimezunguka sana kwasababu nimefanya kazi visiwa vyote na pia wakati wa makuzi.

"Niliajiriwa nikiwa mdogo sana mwaka 1977 nikiwa na miaka 17 hivi, nakumbuka siku ya kwanza kwenda kwenye ajira wakasema rudi nyumbani hapa tutakuwa tunafanya Child Labour, nikarudi nyumbani nikaa miezi sita halafu ndio wakaniita tena,"ameyasema hayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo Januari 27,2022 katika mahojiano na TBC.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news