SIMULIZI MARIDHAWA KUHUSU TEHAMA KUTOKA CHUO KIKUU HURIA TANZANIA

SIKU ya tarehe 11th Desemba 2021, Mwalimu Bakari Kombo Bakari wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kituo cha Pemba  alihudhuria na kushiriki kongamano la Kiswahili la Baraza la Kiswahili Zanzibar (BAKIZA). 
Picha na Mtandao

Miongoni mwa mada zilizowasilishwa ni MATUMIZI YATEHAMA KATIKA KUENDELEZA KISWAHILI DUNIANI. 

Ilidaiwa kwamba, matumizi ya TEHAMA ni chanya kwa vijana tu walio katika X-Generation na ni hasi kabisa kwa wazee wa Y-Generation. 

Wakati wa kuchangia hoja Mwalimu Kombo alisema kwamba wazo lisemalo kuwa TEHAMA ni kwa vijana pekee halina mashiko, kwani Chuo Kikuu Huria Tanzania ni taasisi yenye wazee wengi zaidi, lakini inaongoza kwenye matumizi ya TEHAMA hapa nchini na kote Afrika kwa jumla. DUNIANI pia nafasi ya Chuo Kikuu Huria kwenye matumizi ya TEHAMA ni nzuri pia. 

Kimsingi, Mwalimu Bakari Kombo yeye mwenyewe ni mzee wa miaka 59, lakini ni miongoni mwa watumiaji bora sana wa TEHAMA. 

Pia alisema wapo wahadhiri waandamizi na Maprofessa wana zaidi ya miaka sitini wanatumia TEHAMA tena kwa ufanisi mkubwa. 

Open University of Tanzania inafundisha kwa njia nyingi za teknolojia ya kileo kama kupitia ZOOM, Moodle Platform, You Tube, What's App, Telegram na Email kutaja kwa uchache.

Wahidhiri wote wa chuo wakiwemo wazee wanafanya kazi hii kwa ufanisi mkubwa sana. Aonavyo mwalimu Kombo TEHAMA ni ya wazee na vijana. Isihusishwe na umri wa mtu.

Wasalaam,

Mwalimu  Bakari Kombo

Chuo Kikuu Huria cha Tanzania

Chakechake-Pemba

8/1/2022

Post a Comment

0 Comments