Spika Ndugai amuomba radhi Rais Samia

NA GODFREY NNKO

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Job Ndugai amemuomba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan iwapo kwa namna moja au nyingine ametoa neno la kumvunja moyo kupitia uongozi wake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akiteta jambo na Spika wa Bunge, Job Ndugai hivi karibuni. (Picha na Maktaba).

"Binafsi yangu popote pale ambapo nilihisiwa labda kwa namna moja ama nyingine nimetoa neno la kumvunja moyo Rais wetu na akavunjika moyo nitumie fursa hii kumuomba radhi Mheshimiwa Rais na Watanzania wote, haliwezi kutokea halitotokea na sio rahisi jambo hilo kutokea, 

"Rais ndiye Kiongozi Mkuu, tumuheshimu pekee yake hatoweza tumsaidie kwasababu pamoja tunaweza kwenda mbali zaidi. Wabunge mtawasikia wapo na Rais, na sisi wote tunatekeleza sera na Ilani za CCM hatugombani hata siku moja, lakini wapo watu ambao wangependa kupita katikati na kutusambaratisha, Watu hao washindwe na walegee;

Mheshimiwa Spika Ndugai ameyasema hayo leo Januari 3,2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma.

"Juzi tarehe 26 (Desemba 26,2021) nilikuwa kwenye shughuli nikazungumza baadhi ya mambo baadaye ikatengenezwa clip na baadhi ya watu wakakata baadhi ya mambo wakawasilisha ujumbe nusu ambao umesababisha mjadala mkubwa katika nchi yetu, mjadala ule umesababisha usumbufu wa hapa na pale nimeona tukutane pamoja na mambo mengine niweke sawa jambo hilo lilivyokuwa.

"Nyinyi waandishi mnaweza kufuatilia mkapata mkanda mzima, hapakuwa na jambo la kukashfu au kudharau juhudi zozote za Serikali, Serikali ni Baba yetu, Serikali ni Mama yetu tunahitaji Serikali na tunaiunga mkono,"amesema Mheshimiwa Ndugai.

Amesema, katika mazungumzo hayo aliwataka wenzake pamoja na mambo mengine kujiimarisha kiuchumi, "tulipe kodi na tulipe tozo ili tuisaidie Serikali yetu katika kujitegemea zaidi na sisi kama nchi kujitegemea zaidi na nikaeleza kwa nini sisi Wabunge tulipitisha jambo hili la tozo na nikasema endapo wenzetu mnatuona Wabunge tulifanya jambo baya kupitisha jambo hili basi mtatuhukumu huko mbele, wabunge sikumaanisha taasisi nyingine yoyote,"amefafanua Mheshimiwa Ndugai.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news