Tanzania yafikiwa na Programu ya UEFA ya Maendeleo ya Mpira wa Miguu (UEFA Assist)


NA MWANDISHI DIRAMAKINI

TANZANIA imepata bahati ya kufikiwa na Programu ya UEFA ya Maendeleo ya Mpira wa Miguu (UEFA Assist) ambapo imeandaliwa semina maalum yenye lengo la kuboresha Ligi za Tanzania na Uendeshaji wa Mashindano nchini.
Kwa mujibu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), programu hiyo ilianza Novemba 2021 kwa zoezi la kukusanya maoni ya wadau mbalimbali wakiwemo makocha, wachezaji, Wanahabari, viongozi wa Shirikisho na Bodi ya Ligi, viongozi wa klabu, wadhamini na washabiki.

Hatua ya pili ya Programu hiyo ni semina ambayo itaendeshwa na maafisa wa UEFA Assist kwenye hoteli ya Golden Tulip mkoani Dar es salaam kuanzia Januari 10 hadi 15, 2022.

Washiriki wa semina hiyo ni viongozi na maafisa wa TFF na Bodi ya Ligi, viongozi wa klabu za Ligi Kuu (Mwenyekiti/Rais, Katibu/CEO na Afisa wa Fedha na Mipango).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news