TANZIA: Ajali ya gari msafara wa RC yaua waandishi, maafisa habari Mwanza

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, Bw. Emmanuel Luponya Sherembi, amehairisha ghafla ratiba ya ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Mhandisi Robert Gabriel kwa ajili ya kukabidhi miradi baada ya ajali iliyotokea saa chache na kusababisha vifo.
"Mkurugenzi Mtendaji anasikitika kuwafahamisha kuwa, ratiba ya ziara ya leo ya kukabidhi miradi yetu kwa Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza imeahirishwa ghafla.

"Hii ni kutokana na ajali mbaya iliyoukumba msafara wa Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wakati akiwa anakuja ambapo gari lilokuwa limebeba kikosi cha waandishi wa habari limegongana na Hiace uso kwa uso maeneo ya Busega.

"Taarifa zinasema kuwa watu watano wamepoteza maisha ambao inasemekana kuwa ni waandishi na maafisa habari ndani ya mkoa wetu na pia inasemekana kuwa mojawapo ya waliofariki ni pamoja na ofisa habari na mahusiano wetu, Bw.Stephen Msengi.

"Taarifa zaidi zitaendelea kutolewa na kuthibitishwa. Kufuatia hali hiyo, uongozi wa mkoa na wilaya umeamua kusitisha ratiba ya ziara hii hadi siku nyingine itakayopangwa.Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe. Amen,"imeeleza taarifa kutoka ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji huyo iliyoonwa na DIRAMAKINI BLOG.

Awali, Edwin Soko ambaye ni Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani Mwanza amebainisha kutokea kwa ajali hiyo

"Nineongea na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ndugu Gabriel (Mhandisi Robert Gabriel) amethibitisha kupokea taarifa za watu watano waliokuwa kwenye gari hilo lililobeba waandishi kufariki.Majina ya wenzetu hao tutayatoa kadri tutakavyofuatilia.

"Kwa sasa Mkuu wa Mkoa nae anaelekea eneo la tukio nasi pia tunajipanga kwenda eneo la tukio.Naomba tuwe watulivu kwa wakati huu, wakati team yetu na ya Mkuu wa Mkoa tunafuatilia tukio hilo,"amefafanua Soko.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news