TAWALA TATU NDANI YA FAMILIA

NA MWANDISHI MAALUM

KATIKA Familia kuna vipindi vitatu ambavyo kila kipindi kinamtawala wake. Na kila utawala unaathari ndani ya familia. Mara nyingi utawala wa kwanza ndio hutoa mwelekeo wa familia husika.
 
Picha na Intaneti.

Zifuatazo ni tawala zinazotokea ndani ya familia nyingi;

1. UTAWALA WA BABA

Hiki ni kipindi ambacho mwanaume huwa katika ufalme wake. Kipindi hiki ndicho Baba huwa kauli ya mwisho ndani ya familia. Pia Baba ndio nguzo muhimu ndani ya nyumba katika awamu hii ya kwanza. 
 
Yeye ndiye hutoa muelekeo wa Familia kuwa itakuwa ya aina gani mbeleni. Utawala huu mara nyingi unachangamoto za kiuchumi na kimahusiano kwani Baba bado damu inachemka. 
 
Huanza umri wa miaka 18-49. Kuanzia siku ya uchumba mpaka ndoa. Baba unatakiwa uilee familia kwa upendo, kwani usipofanya hivyo madhara yake utayaona kwenye awamu ya pili ambayo Mama ndiye huingia utawalani. 
 
Ifundishe familia yako kuwa na umoja na ushirikiano. Vinginevyo cha moto kinakuja kwenye tawala mbili zitakazofuata baada yako.

2. UTAWALA WA MAMA

Kipindi hiki huanza mwanaume akiwa na miaka 50 mpaka 65. Hapa mama ndiye huwa na mwelekeo wa Familia. 
 
Yeye ndio nguzo muhimu kwa familia husika. Utawala wake kwa kiasi kikubwa unaimarishwa na nguvu kutoka kwa Watoto ambao muda huo ndio wanamaliza chuo na wanaanza kujitegemea. 
 
Mama hapa kama aliteseka au hakupata upendo kwenye utawala wa kwanza basi muda huu ndio wa yeye kulipa kisasi. 
 
Na kama alipata mapenzi basi hulipa fadhila. Utawala huu mwanaume huweza pata manyanyaso kama sio kuuawa kabisa. 
 
Umri huu ni hatari sana kwa utawala wa kwanza kama haukuwa na haki na usawa. Ila ni kipindi kizuri sana ikiwa utawala wa kwanza ulikuwa 'fair' kwani ni muda wa kula matunda ya ujanani.

3. UTAWALA WA WATOTO

Hiki ni kipindi ambacho watoto wameoa na kuolewa na wanafamilia zao. Kipindi hiki watoto ndio huwa na maamuzi ya kila kitu ndani ya familia. Wao ndio wenye muelekeo wa familia. 
 
Mara nyingi utawala huu huungana na Mama hasa ikiwa Baba alikuwa mkorofi kwenye utawala wake. Pia kama Baba hakuijenga familia iwe na umoja na upendo. 
 
Utawala huu wakati mwingine, humuamisha mtawala wa pili na kuishi naye kwa usalama wake zaidi. Utawala huu hudondosha rasmi Familia hiyo na inapotea katika ramani. Utawala huu huzingirwa na Vifo vya utawala wa Kwanza au utawala wa pili.

Mwisho, Watu waishi kwa Upendo katika familia kila mmoja aingiapo kwenye utawala wake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news