Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) inavyotekeleza majukumu yanayogusa maisha ya kila siku nchini

NA MWANDISHI MAALUM-TAEC

MIONZI inafaida nyingi kwa maendeleo na ustawi katika Jamii inatumika kwenye sekta mbalimbali ikiwemo afya, kilimo, mifugo, ujenzi, maji, nishati na viwanda.
Pamoja na kuwa na faida nyingi, lakini isipotumika inayotakiwa inaweza kuingia katika mnyororo wa chakula ambao ni hatari kwa afya ya binadamu na wanyama.

Kwa kutambua umuhimu wa mionzi ndio maana Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge namba 7 ya mwaka 2003 yenye dhima ya kusimamia na kudhibiti matumizi salama ya mionzi ili kulinda umma, wafanyakazi pamoja na mazingira dhidi ya madhara ya mionzi na kuhamasisha matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia kwa maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi.

TAEC imekuwa ikitekekeza miradi mbalimbali ya kitaifa katika sekta saba kwa kutumia teknolojia ya nyuklia.

Peter Ngamilo Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano kutoka TAEC, akiwa katika maonesho ya mapinduzi yanayoendelea viwanja vya Maisara jijini Zanzibar anasema, katika Sekta ya Kilimo mazao ya mpunga, mahindi na mtama yamekuwa yakikumbwa na changamoto mbalimbali ikiwemo magonjwa.

Mojawapo ya magonjwa ambayo yameathiri kwa kiasi kikubwa uzalishaji wa mpunga nchini ni ugonjwa ujulikanao kitaalamu kama "Yello Mottle Vírus (RYMV).

Anasema, Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani (IAEA) kwa kushirikiana na Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Zanzibar (ZARI) pamoja na Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) zinatekekeza mradi unaotumia teknolojia ya nyuklia ambapo kupitia mradi huo tafiti zilifanyika kupata mbegu bora aina ya SUPA BC ambayo inahimili maradhi pamoja na ukame.

Anasema, IAEA na TAEC imeendelea kuboresha mbegu za mahindi na shairi katika Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Seliani Arusha kwa kutumia teknolojia ya nyuklia ambapo mradi huo umesaidia kutafiti na kupata mbegu bora za mahindi na shairi ambazo zinahimili magonjwa, ukame na kutoa mavuno mengi.

Kwa upande wa sekta ya afya, anasema mwaka 2012 Tanzania iliripotiwa kuwa na wagonjwa wapya wa saratani 33,884 na katika mwaka huo huo wagonjwa 23, 648 walifariki kwa ugonjwa huo, hiyo inaonyesha kwamba idadi kubwa ya wagonjwa wa saratani hupoteza maisha na vifo vya saratani ni asilimia 5.9 ya vifo vyote hapa nchini.

Anasema, IAEA na TAEC imeendelea kuvisaidia kwa kuvipatia vifaa vya kisasa vya matibabu ya saratani kwa njia ya mionzi vituo vya matibabu ya saratani vya Ocean Road jijini Dar es Salaam na Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Ziwa Bugando Mwanza ambapo vituo hivyo viwili vinahitaji uimarishwaji mkubwa na upanuzi.

Aidha, IAEA iliunga mkono juhudi za serikali za kuanzisha Mkakati wa Taifa wa Kupambana na Maradhi ya Saratani (NCCS) 2013-2022.

Anataja mradi mwingine ni lishe ya binadamu ambapo TAEC kwa kushirikiana na IAEA pamoja na Wizara ya Afya na Taasisi ya Chakula na Lishe inaendelea na utafiti unaotumia teknolojia ya nyuklia kuchunguza matatizo ya lishe kwa watoto wadogo

Anasema, teknolojia hiyo inatoa taarifa sahihi za kiuchunguzi ukilinganisha na matumizi ya njia za asili.

Anasema, TAEC na Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela zipo katika mchakato wa kuanzisha shule ya Sayansi na Teknolojia ya Nyuklia ili kutoa elimu ya kiwango cha juu katika nyanja mbalimbali za matumizi ya teknolojia ya Nyuklia (NT).

"Hii yote ni katika kuunga mkono juhudi za serikali za kuhamasisha matumizi ya teknolojia hapa nchini ili kuleta maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kukuza sekta ya viwanda,"amesema.

Anasema kupitia mradi wa Taifa wa "URT0007"itasaidia kujenga uwezo wa wakufunzi ili wabobee katika fani ya Sayansi ya Nyuklia ambapo Taasisi ya Nelson Mandela (NM-AIST) inayoongoza kwa utoaji wa shahada za uzamili (MSc) na uzamivu (PhD) inaendesha mafunzo hayo kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambacho nacho kinatoa elimu ya Sayansi ya Nyuklia ingawa kimeelemewa kutokana na ukosefu wa vifaa vya utafiti. 

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news