Uhusiano wa Tanzania, Morocco, Oman kuneemesha wengi

NA MWANDISHI MAALUM 

SERIKALI ya Tanzania na Morocco zimekubaliana kuimarisha ushirikiano katika nyanja za biashara na uwekezaji, elimu, utalii, uwezeshaji wa kiuchumi kwa wanawake na vijana.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akishiriki mkutano wake na Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco Bw. Nasser Bourita. Mkutano huo umefanyika kwa njia ya mtandao. (Picha zote na WMNUAM)

Makubaliano hayo yamefikiwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi, Liberata Mulamula (Mb) pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco, Bw. Nasser Bourita walipofanya mkutano wa kwa njia ya mtandao. Balozi Mulamula ameshiriki katika mkutano huo akiwa katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akifuatilia mkutano.

“Tumezungumzia masuala ya kuimarisha uhusiano wetu baina ya Tanzania na Morocco na tumepitia makubaliano yaliyofikiwa wakati wa ziara ya Mfalme wa Morocco alipotembelea Tanzania mwaka 2016 pamoja na kuangalia mikataba mbalimbali iliyotiwa saini wakati wa ziara ya Mfalme wa Morocco (Mfalme wa Morocco, Mohammed VI), lakini pia tumejadili umuhimu wa kuwa na Tume ya Pamoja ya Ushirikiano,”amesema Balozi Mulamula. 
Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco Bw. Nasser Bourita akimsikiliza Balozi Mulamula (hayupo pichani) katika mkutano uliofanyika kwa njia ya mtandao.

Katika mkutano huo, viongozi hao wamejadili na kukubaliana kuimarisha ushirikiano wa karibu katika sekta za biashara na uwekezaji, utalii, elimu hasa katika kuongeza idadi ya ufadhili wa masomo kwa watanzania kutoka wanafunzi 30 hadi 50. 

“Morocco ni nchi inayopata watalii wengi, hivyo tumekubaliana kushirikiana kwa karibu zaidi ili kuweza kupata uzoefu ni njia gani wanatumia katika kukuza sekta ya utalii,”ameongeza Balozi Mulamula. 
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akimueleza jambo Kaimu Balozi wa Oman nchini, Dkt. Salim Saif Al Harbi walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Katika tukio jingine, Balozi Mulamula amekutana na kufanya mazungumzo na Kaimu Balozi wa Oman nchini Dkt. Salim Saif Al Harbi katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam. 
Kikao baina ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula na Kaimu Balozi wa Oman nchini Dkt. Salim Saif Al Harbi kikiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam

Mazungumzo ya viongozi hao yamelenga kujadilia masuala mbalimbali ya kuendeleza na kuimarisha ushirikiano uliopo baina ya Serikali ya Tanzania na Oman.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news