Wananchi wavutiwa na kazi za BoT katika Tamasha la Nane la Mapinduzi jijini Zanzibar

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

BANDA la Benki Kuu ya Tanzania (BoT) limeendelea kuwa kivutio kwa wananchi mbalimbali kutoka ndani na nje ya Jiji la Zanzibar ambao wanafika kwa ajili ya kupata elimu kuhusu kazi na majukumu ya msingi ya Benki Kuu ya Tanzania.
Wananchi wakiendelea kupata elimu katika banda la Benki Kuu ya Tanzania jijini Zanzibar. (Picha zote na BoT).

Ni katika Tamasha la Nane la Mapinduzi linalobebwa na kauli mbiu "Teknolojia na Ubunifu katika Ukuaji wa Biashara", ambalo linaendelea jijini Zanzibar. Tamasha hilo linatarajiwa kumalizika Januari 15, 2022.
Tamasha hilo ambalo linafanyika katika Viwanja vya Maisara jijini Zanzibar wataalamu mbalimbali kutoka BoT wanatoa elimu kuhusu kazi na majukumu ya msingi ya BoT kwa wananchi wanaotembelea banda lao.
 
 Majukumu ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT)

Jukumu la msingi la Benki Kuu ya Tanzania ni kuandaa na kutekeleza sera ya fedha inayolenga kudhibiti mfumuko wa bei na kujenga mfumo wa fedha ulio imara na unaofaa kwa ukuaji endelevu wa uchumi wa taifa.

Majukumu mengine ya Benki Kuu ya Tanzania;

>Kutoa sarafu ya nchi ambayo ni Shilingi ya Tanzania
>Kusimamia na kudhibiti mabenki na taasisi za fedha
>Kusimamia na kudhibiti mifumo ya malipo nchini.
>Kusimamia akiba ya nchi ikiwemo fedha za kigeni
>Benki ya Serikali
>Benki ya Mabenki; na
>Kutoa ushauri juu ya masuala ya uchumi na fedha kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Post a Comment

0 Comments