Wanaume watajwa kushiriki kikamilifu uchimbaji madini

NA TITO MSELEM-WM

WAZIRI wa Madini, Dkt. Doto Biteko amesema kubwa Tafiti zinaonesha uchimbaji wa madini kwa miaka mingi umekuwa ukifanywa na wanaume kuliko wanawake ambapo kati ya wachimbaji wadogo wa madini 100, wanawake ni 7 peke yake.
Waziri Biteko ameyasema hayo alipotembelea mgodi wa madini ya vito uliopo katika kijiji cha Nhalo wilayani Gairo mkoa wa Morogoro. 

Dkt. Biteko amesema kuwa, kipindi cha nyuma wachimbaji wadogo wote nchini walikuwa wanachangia chini ya asilimia 4 kwenye pato la madini lakini kwa sasa wachimbaji wadogo wanachangia zaidi ya asilimia 30 katika pato hilo.
Kufuatia hatua hiyo, Sekta ya Madini inauhakika wa kufikia asilimia 10 ya mchango wake kwenye pato la taifa ifikapo mwaka 2025.
Sambamba na hayo, Dkt. Biteko amesema Serikali kupitia Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) limeingia mkataba na Benki mbalimbali nchini ili kuwadhamini wachimbaji wadogo waweze kukopesheka ili wachimbe kwa tija.

Aidha, Dkt. Biteko amewatoa hofu wachimbaji wadogo wa madini ya vito juu ya upatikanaji wa soko la uhakika la madini kutokana na dunia kukumbwa na janga la Uviko-19 lililopelekea soko hilo kuyumba.

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Gairo Jabiri Makame amempongeza Dkt. Biteko kwa kufanya ziara wilayani Gairo ambapo amesema ujio wa Waziri wa Madini unaenda kuzimaliza changamoto zinazo wakabili wadau wa madini wilayani humo.
"Tunaomba utufikishie salamu zetu kwa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea maendeleo katika Wilaya yetu ya Gairo, mwambie tunamshukuru sana," amesema Makame.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news