Warembo wa SC wawakosesha raha wale wa Yanga SC, wakubali 4-1

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

WAREMBO wa Klabu ya Simba ambao ni mabingwa watetezi, Simba Queens wamewachakaza watani wao, Yanga Princess.
Ni baada ya ushindi wa mabao 4-1 Januari 8,2022 katika mtanange wa Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite 2021/2022 ndani ya dimba la  Benjamin Mkapa katika Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam.
Aisha Djafar dakika ya saba na 82 na Opa Clement dakika ya 54 na 72 ndiyo waliopeleka maumivu kwa Yanga Princess.
Huku bao pekee la Yanga Princess likifungwa na Aisha Masaka kwa penalti dakika ya 76.

Chini ni msimamo wa Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite 2021/2022.

Post a Comment

0 Comments