Waziri Bashe:Hakuna mwananchi atakayekufa kwa njaa Tanzania

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

SERIKALI imewahakikishia wananchi kuwa, hakuna mtu atakayekufa kutokana na njaa ndani ya Tanzania. 
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Hussein Bashe amesema, Serikali ina akiba ya chakula inayokidhi mahitaji ya wananchi watakaokuwa na upungufu wa chakula.

Aidha, Waziri Bashe amefafanua kuwa, Serikali ina akiba ya chakula zaidi ya tani laki mbili ambazo zitatoshelaza mahitaji ya wananchi katika mikoa itakayopungukiwa chakula.

Katika kuhakikisha kuwa chakula kinawafikia walengwa kwa bei nafuu, Serikali kupitia Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), itaweka vituo katika ngazi ya halmashauri na kuwauzia wananchi chakula kwa bei ya rejareja.

Kuhusu changamoto ya kupanda kwa bei ya mbolea, Mhe. Bashe amesema, tatizo hilo limetokana na mabadiliko ya bei za mbolea katika soko la Dunia.

Aidha,kuhusu hatua zilizochukuliwa na Serikali kutatua changamoto ya bei ya,Mhe. Bashe mesema atakaa pamoja na viongozi wa kampuni kumi za waagizaji wa mbolea ili kujadiliana namna bora ya kutatua changamoto hiyo. 

Aidha, Mheshimiwa Bashe amesma kikao chake na waagizaji wa mbolea kinalenga kutafuta ufumbuzi wa muda mrefu wa tatizo la bei ya mbolea kama alivyoelekeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news