Waziri Bashungwa ataja vigezo vinavyotumika kuwapima wakuu wa wilaya, wakurugenzi watendaji nchini

NA ANGELA MSIMBIRA, OR-TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mheshimiwa Innocent Bashungwa amesema kuwa Wakurugenzi wa Halmashauri na Wakuu wa Wilaya watapimwa kutokana na utendaji kazi wao wa kuhakikisha wanatatua kero za wananchi.
Akiongea na viongozi wa Mkoa wa Njombe,Waziri Bashungwa amesema moja ya kigezo cha kuwapima Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya ni kasi ya ukusanyaji wa mapato katika halmashauri.

Pia amewaagiza kuhakikisha wanaongeza kasi ya ukusanyaji wa mapato.

Ameongeza kuwa, fedha nyingi zinatolewa na Serikali kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo, hivyo ni wajibu wa viongozi hao kuhakikisha wanasimamia matumizi ya fedha hizo, "hivyo nitoe wito kwa Wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanasimamia matumizi ya fedha hizo kwa uaminifu.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ametuamini vijana katika kumsaidia kutekeleza majukumu yake ya kuwahudumia wananchi, hivyo wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya tusimuangushe na mimi nikiwa ni Waziri mwenye dhamana sitakubali kumuangusha,” amesisitiza Waziri Bashungwa.

Waziri Bashungwa amesisitiza Wakurugenzi  wanapaswa kuhakikisha wanajibu hoja za Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa asilimia 100 na kuhakikisha fedha zinazokusanywa zinawekwa benki kwa wakati na kuacha tabia ya kutumia fedha mbichi.

Ameongeza kuwa, kigezo kingine ni utoaji wa mikopo ya asilimia kumi kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.

Pia amewataka kuhakikisha fedha inayotolewa inaenda kwenye miradi yenye tija ya kuwasaidia waliopewa, amewataa viongozi hao kutoa ushauri wa namna bora ya kukusanya fedha zilizotolewa.

Aidha, amewaagiza wakuu wa mikoa wote nchini kuhakikisha wanasimamia utoaji wa mikopo kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu na kuhakikisha fedha hizo zinaenda kwenye miradi yenye tija na kama kuna ujanja unaofanywa na Halmashauri au idara inayoshughulikana mikopo wafuatilie na kutoa taarifa Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kuwa hicho pia ni kigezo kingine cha kuwapima Wakurugenzi katika Halmashauri kwa kuangalia wanasimamia vipi utoaji wa mikopo ya asilimia 10.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news