Waziri Bashungwa ateua 12 Tamasha la Serengeti

NA GODFREY NNKO

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Innocent Bashungwa ameteua wajumbe mbalimbali wa Kamati ya Tamasha la Serengeti (Serengeti Music Festival).

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt.Hassan Abbasi, Januari Mosi,2021.

Kupitia taarifa hiyo, Katibu Mkuu ameeleza kuwa, uteuzi wa Waziri Bashungwa utasaidia kuratibu tamasha hilo la Kitaifa lenye dhima ya kuwaleta wasanii pamoja.

Pia ameeleza kuwa, tamasha hilo ni muunganiko wa tukio la kimkakati la sekta ya sanaa na utalii katika kuitangaza nchi yetu.

Wajumbe walioteuliwa na Waziri ni pamoja na Dkt.Emmanuel Ishengoma ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Sanaa ambapo atawakuwa Mwenyekiti.

Wajumbe ni Mniko Matiko ambaye ni Kaimu Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), Addo Novemba ambaye ni Rais wa Shirikisho la Muziki nchini, Mkuwe Burhan Mandi (B-Dozen) kutoka EFM, Omary Tambwe (LlyOmmy) kutoka Wasafi, Tatenda Joseph Nyawo kutoka A FM Radio Dodoma.

Wajumbe wengine ni Hamza Balla Shareeph kutoka Tigo, Neema Rose Singo kutoka NBC, Jadi Ngwale kutoka CRDB, Mercy Nyange kutoka NMB na Paschal Shelutete kutoka TANAPA.

"Kamati hii inaanza utekelezaji wa majukumu yake kwa kushirikiana na waratibu wa tamasha hilo mara moja,"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo.
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mheshimiwa Innocent Bashungwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news