Waziri Dkt.Ndumbaro:Sekta ya Misitu na Nyuki kuendelea kuchangia zaidi pato la Taifa

NA HAPPINESS SHAYO-WM

SERIKALI kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imepanga kuibua mbinu mpya zitakazoiwezesha Sekta ya Misitu na Nyuki kuongeza mapato katika pato la Taifa.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akizungumza na menejimenti ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika kikao kilichofanyika Katika ukumbi wa Chuo Cha Taifa cha Utalii tarehe 11 Januari 2022 Jijini Dar es Salaam.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro alipofanya kikao na menejimenti ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwenye ukumbi wa Chuo cha Taifa cha Utalii tarehe 11 Januari 2022 jijini Dar es Salaam.

“Tunategemea tuje na mbinu zote za kuongeza mchango wa Sekta ya Misitu na Nyuki kwenye uchumi wa nchi na mojawapo ya mchango huo ni biashara ya hewa ya ukaa (Forest Carbone Trade)”.
Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro (Mb) akizungumza na menejimenti ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika kikao kilichofanyika Katika ukumbi wa Chuo Cha Taifa cha Utalii tarehe 11 Januari 2022 Jijini Dar es Salaam. (kulia) ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja (Mb), na (kushoto) ni Mtendaji Mkuu wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)). Prof.Dos Santos Silayo.

Amesema Wizara ya Maliasili na Utalii ina mamlaka kamili kwenye kusimamia biashara ya hewa ya ukaa kwa sababu sheria na sera ya misitu iko chini ya Wizara hiyo.

Kwa upande wake Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja ameishauri menejimenti ya TFS kuhakikisha inatekeleza mpango wa biashara ya hewa ya ukaa kwa wakati kwa sababu kwa kufanya hivyo itasaidia kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya maliasili na utalii.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Mary Masanja (Mb) akizungumza na menejimenti ya Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) katika kikao kilichofanyika Katika ukumbi wa Chuo Cha Taifa cha Utalii tarehe 11 Januari 2022Jijini Dar es Salaam. (Kushoto) ni Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro akifuatilia.

Pia, amewataka watendaji hao kufanya kazi kwa kasi ili kuleta matokeo chanya.

“Tuendane na kasi ya utekelezaji wa mpango huu kwa sababu sisi tunapimwa pale tunapoonyesha matokeo chanya kama alivyosema Mhe. Waziri tunaangaliwa tumeingiza fedha kiasi gani na watalii kiasi gani,” Mhe. Masanja amesisitiza.

Mtendaji Mkuu wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS)). Prof.Dos Santos Silayo akitoa ufafanuzi wa namna biashara ya ukaa inavyoweza katika kikao kilichofanyika Katika ukumbi wa Chuo Cha Taifa cha Utalii Jijini Dar es Salaam.

Naye, Mtendaji Mkuu, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS), Prof. Dos Santos Silayo amewapongeza kwa kuteuliwa kwa mara nyingine kuiongoza Wizara na kuahidi kutoa ushirikiano na kuhakikisha anasimamia utekelezaji wa maagizo yote yaliyotolewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news