WAZIRI MASAUNI AIPONGEZA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI KWA KAZI NZURI INAYOFANYA

NA MWANDISHI MAALUM

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Yusuph Masauni, ameipongeza Menejimenti na Watumishi wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, kwa kazi nzuri ambazo wameendelea kuzitekeleza katika Wizara hii.
Mhandisi Masauni ameyasema hayo leo wakati akipokelewa rasmi katika Ofisi za Wizara hiyo Mtumba jijini Doodoma, baada tu ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kushika wadhifa wa Waziri wa Mambo ya Ndani.

“Ni Imani yangu tutaendelea kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja kwa maslahi mapana ya Taifa letu, mara zote ushirikiano ndio unaoweza kufanikisha kuondoa changamoto mbalimbali zinazotukabili’ amesisitiza Mhandisi Masauni.
Waziri Masauni amewataka watendaji na watumishi wa Wizara hiyo, kutosita kutoa ushauri katika jambo lolote ambalo likitekelezwa litaleta ufanisi na mafanikio ya kiutendaji katika Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Amesisitiza kuwa, kufanya kazi kwa upendo na ushirikiano ndio msingi wa mafanikio katika kutekeleza majukumu yaliyo mbele yetu kwa ufanisi mkubwa.
Kwa upande wake Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Jumanne Sagini, amesisitiza Watumishi wote kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuweza kutatua changamoto zozote zile zinazoikabili Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news