Yaliyojiri Kilimanjaro ni zaidi ya Tamasha la Utamaduni

NA GODFREY NNKO

SERIKALI ya Awamu ya Sita chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan imetajwa kuvunja rekodi kwa kuelekeza fedha nyingi za maendeleo mkoani Kilimanjaro kwa kipindi cha miezi sita tu.
Hayo yamesemwa leo Januari 22, 2022 na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mheshimiwa Stephen Kagaigai katika uwanja wa Chuo Kikuu cha Ushirika (MoCU) wakati wa uzinduzi wa Tamasha la Utamaduni mkoa Kilimanjaro.

Katika tamasha hilo ambalo, Mheshimiwa Rais Samia alikuwa mgeni rasmi, Mheshimiwa Kagaigai amesema, katika kipindi cha Julai hadi Desemba 2021, mkoa huo umepokea shilingi Bilioni 57.39 sawa na asilimia 40 ya bajeti yote ya maendeleo.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe.Steven Kigaigai akitoa hotuba yake katika Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Kilimanjaro lilofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro lililofanyika leo tarehe 22/01/2022 na kuhudhuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Chifu Hangaya Mhe.Samia Suluhu Hassan ambaye pia alikuwa mgeni rasmi.

Amesema, hicho ni kiwango kikubwa cha fedha za maendeleo kuwahi kupokelewa mkoani humo katika nusu ya kwanza ya mwaka wa fedha wa Serikali. 

"Kwa niaba ya wananchi wa Kilimanjaro tunakushukuru sana,”amesema Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mheshimiwa Kagaigai mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Mheshimiwa Kagaigai amesema, mkoa huo ulipokea shilingi Bilioni 7.88 ambazo ni sehemu ya mkopo wa shilingi trilioni 1.3 kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) kwa ajili ya Ustawi na Mapambano Dhidi ya Ugonjwa wa UVIKO-19.
Naibu Waziri wa Sanaa,Utamaduni na Michezo Mhe.Paulina Gekul akitoa hotuba yake katika Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Kilimanjaro lilofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro lililofanyika leo tarehe 22/01/2022 na kuhudhuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Chifu Hangaya Mhe.Samia Suluhu Hassan ambaye pia alikuwa mgeni rasmi.

Pia amesema, mkoa huo ulipokea shilingi bilioni 2.48 zinazotokana na tozo kwenye miamala ya simu, shilingi bilioni 18 za ruzuku ya maendeleo kwa Serikali za mitaa na pia mkoa ulipata shilingi bilioni 4.2 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya za kata mkoani humo.

Mheshimiwa Kagaigai ameendelea kufafanua kuwa,mkoa huo ulipokea shilingi milioni 418.1 ambazo ni fedha za mpango wa matokeo, shilingi bilioni 22.44 kwa ajili ya matengenezo na ukarabati wa barabara na ukapokea shilingi bilioni 1.9 kwa ajili ya miundombinu ya maji katika mkoa huo.

Amesema, fedha zote zilizopokelewa zimeelekezwa kwenye ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya utoaji wa huduma katika sekta za afya, elimu, maji, barabara na madaraja katika maeneo mbalimbali mkoani humo.

Changamoto

Wakati huo huo, Mheshimiwa Kagaigai amesema, mifugo 1,257 imekufaa mkoani Kilimanjaro kutokana kukosa maji na malisho baada ya ukame kukumba eneo maeneo mengi.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai wakati akitoa taarifa ya Mkoa huo kwa Rais Samia Suluhu Hassan ambaye yupo mkoani humo kwa ajili ya kuzindua Tamasha la Utamaduni.

Mheshimiwa Kagaigai mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametaja mifugo iliyokufa kuwa ni ng’ombe 841, kondoo 406 na punda 10.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Chifu Hangaya Mhe.Samia Suluhu Hassani akizungumza katika Tamasha la Utamaduni Mkoa wa Kilimanjaro lililofanyika leo tarehe 22/01/2022 katika Viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro.

"Mweshimiwa Rais, pamoja na mafanikio na kazi mbalimbali za maendeleo zinazoendelea, mkoa tunakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo kutonyesha kwa mvua za vuli, hali ambayo imesababisha ukame na vifo vya mifugo. Uongozi wa mkoa unaendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kukabiliana na hali hiyo,"amesema Mheshimiwa Kagaigai. 

Aidha, amefafanua kuwa, mbali na vifo hivyo vya mifugo, hali ya chakula bado ni nzuri na mkoa unachakula cha kutosha.

Rais Samia

Kwa upande wake Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametumia nafasi hiyo kuwapa pole wananchi wa Mkoa wa Kilimanjaro na mikoa mingine kutokana na ukame ulioikumba mikoa hiyo hususani katika maeneo ya ufugaji uliosababishwa na kuchelewa kunyesha kwa mvua na hivyo kupelekea wananchi kupoteza maelfu ya mifugo.
Baadhi ya viongozi wa Dini Mkoa wa Kilimanjaro wakishiriki Tamasha la Utamaduni mkoa wa Kilimanjaro ambalo limefanyika leo Januari 22,2022 katika viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi mkoani humu ambapo Mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan.

Amewataka wafugaji kushirikiana na Serikali ili kutumia mafunzo wanayoyapata kutokana na janga la ukame kuona namna bora ya kuanza ufugaji wa kisasa usiotegemea mvua katika kupata malisho.

Machifu

Wakati huo huo, Mheshimiwa Rais Samia amewashukuru Machifu wa mkoa huo kwa kuitikia wito alioutoa mkoani Mwanza na kuelekeza mikoa yote nchini kufanya matamasha ya utamaduni kwa lengo la kuendeleza mila, desturi na utamaduni na Taifa letu ili zisipotee.

Amesema, Serikali iliunda wizara mahususi itakayosimamia moja kwa moja shughuli za sanaa, utamaduni na michezo kwa sababu ilitambua umuhimu wa sekta hizo katika kutoa ajira, kukuza uchumi wa nchi na kuitangaza nchi Kimataifa.

Pia, Mheshimiwa Rais Samia ameitaka Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo kuendelea kuratibu, kuvikuza na kuviendeleza vikundi vya burudani za kitamaduni ili vikazalishe kazi za mikono za utamaduni kama vile ufinyanzi, ususi, upishi, uchongaji pamoja na kuhamasisha mashindano ya tambo, tenzi, nahau na ushairi kwa kutumia mila na usarifu wa lugha ya Kiswahili.

Urejeshwaji mafuvu

Pia Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amesema, Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Maliasili na Utalii wanaendelea na majadiliano ya urejeshwaji wa mafuvu ya viongozi wa kimila yaliyochukuliwa na Wakoloni.
Baadhi ya Machifu Mkoa wa Kilimanjaro wakiwa katika Tamasha la Utamaduni mkoa wa Kilimanjaro ambapo mgeni rasmi alikuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Samia Suluhu Hassan. Tamasha hilo limefanyika leo Januari 22,2022 katika Viwanja vya Chuo cha Ushiriki Moshi Mkoani Kilimanjaro.

Ameyasema hayo baada ya Mwenyekiti wa Machifu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Frank Marialle kumuomba urejeshwaji wa mafuvu hayo ili yatumike kuendeleza historia na utalii katika mkoa huo.

"Mmeomba kuyarejesha nchini mafuvu ya machifu yaliyochukuliwa wakati wa ukoloni ili yatumike kuelimisha jamii na shughuli za kitalii, Sserikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Maliasili na Utalii wanaendela na majadiliano ya urejeshwaji wa mafuvu hayo tutakapofanikiwa tutawaarifu," amesema Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Chifu Marialle

Awali Mwenyekiti wa Machifu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Frank Marialle wakati akisoma risala ya umoja wa Machifu mkoani humo ameiomba Serikali kuzisaidia familia ambazo mafuvu ya viongozi wao wa kimila yalichukuliwa na wakoloni hususani Wajerumani ili yarejeshwe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Chifu Hangaya Mhe.Samia Suluhu Hassan akivalishwa vazi la Utamaduni kama ishara ya kukaribishwa katika mkoa wa Kilimanjaro katika Tamasha la Utamaduni la Mkoa wa Kilimanjaro uliofanyika leo tarehe 22/01/2022 katika viwanja vya Chuo cha Ushirika Moshi mkoani Kilimanjaro.

"Ni ili yaweze kurejeshwa na yatumike kuendeleza historia na utalii katika mkoa na kuongeza kipato kwa jamii na Serikali kwa ujumla,"amesema Mwenyekiti huo.

Mhe. Rais Samia amezitaka Wizara zinazoshughulikia utamaduni na utalii kuandaa mkakati wa pamoja wa kuyabaini matamasha ya kimataifa na kimkoa yatakayoboreshwa na kuendeshwa kimkakati ili yaweze kuwavutia wageni kutoka nje na ndani ya nchi na kuitangaza nchi yetu. 

Katika kuendeleza na kuimarisha utamaduni, mila na desturi za kitanzania, Mhe. Rais amesema tayari Serikali imeanzisha kanzi data sahihi inayohusu Machifu, na kwamba Serikali imeanza kuweka taarifa sahihi za Machifu na mchango wao katika kupambana na ukoloni. 

Mhe. Rais Samia pia amesema kuwa Serikali inaendelea kuyabaini maeneo ya kichifu na kimila na kuyatunza ili yawe sehemu za vivutio vya nchi yetu pamoja na kuibua, kuimarisha na kuhifadhi majengo na zana za zamani ili zibaki kuwa vielelezo vya utamaduni wetu. 

Aidha, Mhe. Rais Samia amebainisha kuwa Serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Wizara ya Maliasili na Utalii zinaendelea na majadiliano ya urejeshwaji wa mafuvu ya Machifu yaliyochukuliwa wakati wa ukoloni ili yatumike kuelimisha jamii.
Mhe. Rais Samia amewasihi viongozi wa Machifu kuwahimiza watanzania kujilinda na janga la UVIKO 19 ikiwa ni pamoja na kupata chanjo na kuwahamaisha wananchi kushiriki katika zoezi la Sensa litakalofanyika mwezi Agosti mwaka 2022. 

Katika Tamasha hilo Mhe. Rais Samia ametembelea mabanda ya makabila matatu ya Wachaga, Wapare na Wamasai na kuonesha vitu mbalimbali ikiwemo vyakula vya asili vya makabila hayo pamoja na dawa za asili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news