Yanga SC, Namungo FC watangulia Dar, wenzao Simba SC na Azam FC ni mwendo wa kutafuna mikate na energy Mapinduzi Cup

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MATARAJIO ya Yanga SC na Namungo FC kutwaa Kombe la Mapinduzi yamezimika ghafla baada ya Yanga SC kuchapwa mabao 9-8 na Azam FC.
Ni katika mtanange wa awali uliopigwa katika dimba la Amaan jijini Zanzibar huku uliomalizika muda huu Simba SC ikiwatandika mabao 2-0 Namungo FC.

Meddie Kagere alipachika bao la kuongoza katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Namungo FC.
Bao hilo lilipachikwa dakika ya 14 baada ya kipa wa Namungo, kutema mpira uliopigwa na Papa Ousmane Sakho. Dakika ya 49 ya kipindi cha pili, Papa Sakho aliwanyanyua mashabiki wa Simba kwa bao la pili.

Kwa matokeo hayo sasa, Simba SC itakutana na Azam FC, hivyo itakuwa ni uamuzi wa kila mmoja kuamua kutumia kinywaji chake ambacho anaamini kitampa nguvu.

Ni Azam Energy kwa mikate, maandazi, biscuits na chapati au Mo Energy kwa biscuits za Mo Biscuits, matokeo tutayafahamu Januari 13,2022 katika Fainali Kombe la Mapinduzi hapa dimba la Amaan jijini Zanzibar.

Post a Comment

0 Comments