Yusuph Kileo aongoza kampeni maalum ya kuwalinda watoto dhidi ya habari za upotoshaji na dhuluma za kimtandao jijini Arusha

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

KAMPENI maalum ya kuwalinda watoto dhidi ya habari za upotoshaji na dhuluma za kimtandao imefanyika jijini Arusha.

Lengo ni kuwawezesha watoto kutambua namna bora ya kujilinda mtandaoni dhidi ya uhalifu utokanao na matumizi mabaya ya teknolojia ya mitandao na namna ya kutumia teknolojia hiyo kujipatia manufaa kwa maisha yao ya baadae.
Ukuaji wa matumizi ya TEHAMA unatajwa umepelekea watoto wengi kuwa wahanga wa matukio ya kihalifu mtandao,kwa kudanganywa mitandaoni na kutazama picha za maudhui yasiyowafaa inayowapelekea kupata madhara ya kisaikolojia.

Kampeni hiyo inafanyika katika Shule ya Sekondari ya St.Yuda iliyopo Pembezoni kidogo mwa Jiji la Arusha na imehusisha wanafunzi wa kidato cha tatu hadi cha sita.
Akizungumza katika kampeni hiyo, Mtaalam wa Usalama Mtandao na Uchunguzi wa Makosa ya Kidigitali, Yusuph Kileo amesema kwamba, lengo mahususi la kuandaa kampeni hiyo ni kulisaidia taifa kuandaa vijana wenye uelewa mzuri katika Matumizi ya Mifumo ya TEHAMA ambayo inatajwa kukuwa kwa kasi duniani.

"Matumizi mabaya ya kimtandao kwa watoto yanatajwa kuathiri maisha yao ya baadae kama wanavyobainisha baadhi ya watoto waliopata fursa ya kupatiwa mafunzo ya namna bora ya kutumia mitandao,"amesema.
Inaelezwa kuwa, Tanzania inakabiliwa kwa kiasi kikubwa na changamoto ya wizi wa mitandaoni hivyo kuchangia upotevu wa fedha nyingi kwa siku.

Post a Comment

0 Comments