CCM WAMJULIA HALI PROFESA JAY

NA MWANDISHI MAALUM

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo leo Februari 10, 2022 akiwa ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka wamemjuilia hali aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Mikumi mkoani Morogoro na msanii nguli wa kizazi kipya, Joseph Leonard Haule (Prof. Jay) alieyelazwa hospital ya Taifa Muhimbili akiendelea na matibabu. 
"Tumemuona Ndugu yetu (Prof Jay) hali yake inazidi kuimarika, tumshukuru Mungu lakini niwashukuru madaktari kwa kazi nzuri wanayoifanya ya kumhudumia, pamoja na mchango huu wa kuwezesha matibabu, lakini kwa niaba ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan niwahakikishie tutaendelea kutoa kila aina ya ushirikiano katika kuhakikisha matibabu yanaendelea vyema huku tukiendelea kumuombea apone haraka,"amesema Chongolo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news