Dkt.Chaula azifunda NGOs

NA MWANDISHI MAALUM

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. Zainab Chaula amekutana na Asasi za Kiraia (AZAKI) kutoka mikoa ya Dodoma, Singida na Iringa lengo likiwa ni kujadili juu ya ustawi wa taasisi hizo nchini.
Mkutano huo ulifanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, ukiwa ni utekelezaji wa ombi la Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs), Neema Lugangira kuhusu wizara hiyo kukutana na NGOs za mikoani na ombi hilo aliliwasilisha alipokutana na Katibu Mkuu huyo Januari 24, mwaka huu.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Dkt. Zainab Chaula kushoto akizungumza wakati wa kikao hicho na wa kwanza kulia ni Mbunge wa Viti Maalumu  kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs), Neema Lugangira.
Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs), Neema Lugangira.

Akizungumza wakati wa kikao hicho, Katibu
Mkuu Chaula amesema kikao hicho na mambo mengine kimelenga kupokea changamoto,kutoa elimu ya namna ya kuendesha AZAKI kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu ikiwemo kukabiliana na namna ya kuimarisha sekta hiyo.

Ameongeza kuwa, kikao hicho kimetoa fursa kwa AZAKI kutoka mikoani kutoa maoni yao na kupata uwakilishi katika  vikao na wizara kutokana na kwamba Asasi hizo zimekuwa na mchango mkubwa katika maendeleo ya Tanzania.
Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Asasi za Kiraia Tanzania Bara (NGOs), Neema Lugangira akisistiza jambo wakati wa kikao hicho.

Ambapo zimekuwa zikitoa elimu kwa wananchi kuhusu mipango mbalimbali ya Serikali ikiwemo mabadiliko ya tabia ya nchi, masuala ya kiafya na kidemokrasia.

Akizungumza wakati wa Kikao hicho, Mbunge Neema Lugangira amesema lengo ni kutoa fursa kwa NGOs za mikoani kutoa maoni yao na kupata uwakilishi katika vikao na wizara.
Amesema, pia lengo lengine ni kupokea changamoto, kutoa elimu ya namna ya kuendesha NGOs kwa kufuata sheria na
kanuni na taratibu na kukubaliana namna ya kuimarisha Sekta ya Azaki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news