Dkt.Mkama:Tuache kufanya kazi kwa mazoea

NA ASILA TWAHA-OR TAMISEMI

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dkt.Switbert Mkama amewataka Wakurugenzi kusimamia utekelezaji na ubora wa miradi yote inayotekelezwa katika maeneo yao ili thamani ya fedha ionekane.
Dkt. Mkama ameyasema hayo leo Februari 15,2022 jijini Dodoma katika kikao kazi kilichowakutanisha Wakurungenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Dodoma, lengo likiwa ni kuwakumbusha majukumu yao waliyopewa katika kusimamia na kutoa matokeo chanya yaliyokusidiwa na Serikali katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Akionesha kutokuridhishwa na utendaji kazi wa baadhi ya Wakurugenzi na Wakuu wa Idara kushindwa kutekeleza majukumu yao ya kisheria na kidhamu na kupelekea kushindwa kusimamia miradi kwa waledi amesema hatamvumilia za tabia za namna hiyo.
“Mnatakiwa kusimamia miradi kwa weledi mtambue kuwa ni lengo la miradi hiyo ni kuwawezesha wananchi kupata huduma bora simamieni miradi hiyo kwa makini msilete mazoea kwenye miradi, wengi wenu mnasimamia bila ya kufuata utaratibu,” Dkt.Mkama.

Ameongeza kuwa, "Serikali haitamvumulia mtendaji yoyote ambaye ataenda kinyume na malengo ya Serikali ikiwa taratibu zote mnazifahamu, niwaambie Sheria, Kanuni na Taratibu za kinidhamu zitachukuliwa kwa kiongozi na mtumishi yoyote atakaefanya kazi kwa mazoea na kwenda kinyume na sheria na taratibu za Serikali katika utekelezaji wa miradi inayotekelezwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa,” amesisitiza.
Ameelezea kuwa, baadhi ya halmashuri hazifuati utaratibu katika kufanya taratibu za manunuzi, kubadilisha matumizi ya pesa bila kufuata utaratibu na kutofuata utaratibu wa utoaji wa mikopo ya Serikali kwenye vikundi vya akinamama, vijana na watu wenye ulemavu, hivyo kuwaonya watumishi watakaobainika kwenda kinyume na taratibu kwani hatua kali za kisheria zitachukuliwa.

"Na nitoe rai kwenu watumishi wa umma kuwa hii si tu kwa Wakurugenzi bali ni kwa ngazi zote,”amesema Dkt.Mkama.

Akizungumzia suala la kushuka kwa ukusanyaji wa mapato katika baadhi ya Halmashauri nchini kutokana na kuwenda kinyume na utendaji kazi wa kutokutumia ama kuharibu mashine za ukusanyaji wa mapato, amezielekeza halmashuri hizo kuacha tabia hizo mara moja kwani Serikali haitasita kuchukua hatua.
Kwa upande wake Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Afya), Dkt.Grace Magembe amesisitiza suala la utoaji wa huduma bora kwa wananchi na kukamilisha miradi haraka ili kuwapunguzia wananchi kusafiri umbali mrefu ikufikia huduma za kijamii.

“Nisema tu kama huwezi kuhudumia wananchi maana yake wewe hutoshi kukaa katika kiti ulichokalia sababu Serikali imetuamini ili tusimamie miradi na tuwahudumie wananchi katika utoaji wa huduma bora sasa kama unaona kiti ulichokalia hakikutoshi atapatiwa mtu mwenye uwezo wa kusimamia na kutoa huduma bora kwa wananchi wetu,”amesema Dkt.Grace.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news