EC yaipa Tanzania msaada wa trilioni 1.15/- kugharamia miradi

NA GODFREY NNKO

SERIKALI ya Tanzania imepata msaada wa shilingi trilioni 1.15 sawa na Euro milioni 425 kutoka Kamisheni ya Umoja wa Ulaya (EC) ili kugharamia miradi mbalimbali ya maendeleo.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Februari 18, 2022 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu), Bi.Zuhura Yunus.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa katika mazungumzo na Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya Mhe. Ursula von der Leyen, Brussels nchini Ubelgiji leo Februari 18, 2022. (Picha na Ikulu).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya, Mheshimiwa Ursula von der Leyen ametangaza kiasi hicho cha msaada baada ya kukutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan aliyeko ziarani nchini Ubelgiji.

Aidha taarifa hiyo imefafanua kuwa;

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news