Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira yaipongeza SIDO kwa kuendesha Mfuko wa NEDF kwa mafanikio

NA MWANDISHI MAALUM

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira imelipongeza Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (SIDO) kwa kuendesha Mfuko wa Taifa Kuendeleza Wajasiriamali Wananchi (NEDF) kwa mafanikio na kulitaka shirika hilo kuongeza ubunifu katika kutafuta njia mbalimbali za kutunisha mtaji wa mfuko huo ili kuwawezesha wananchi wengi mijini na vijijini kuanzisha viwanda vidogo vidogo. 
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Mhe. Erick Shigongo (Mb) wa pili kushoto  akitoa maelekezo kwa Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara wakati wa utoaji wa taarifa ya utekelezaji wa Mfuko NEDF kwa Wajumbe wa Kamati hiyo Februari 5, 2022 katika Ukumbi wa Bunge jijini Dodoma. (Picha na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara).

Hayo yamesemwa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Mhe. Erick Shigongo (Mb) wakati wa utoaji wa taarifa ya utekelezaji wa Mfuko wa NEDF kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Februari 5, 2022 katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma. (Picha na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara).
Mmoja wa wajumbe, Mhe. Josephat Gwajima (Mb) akitoa maoni yake katika kikao hicho.(Picha na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara).
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akizungumza katika kikao hicho ambapo  aliihakikishia kamati hiyo kuwa,wizara itakwenda kushughulika maoni waliyoyatoa katika kuboresha na kutunisha Mfuko wa NEDF. (Picha na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara).
Aidha, Wajumbe wa Kamati hiyo walitoa maoni na mapendekezo mbalimbali yanayolenga kuboresha Mfuko wa NEDF hususani katika kutafuta njia za kuongeza fedha za mtaji wa mfuko, utoaji wa mikopo mijini na vijijini kwa kuzingatia makundi maalumu, muundo wa uendeshaji, viwango vya mikopo, vigezo vya kupata mikopo, riba ya mikopo hiyo na ufadhili wa vikundi vya wajasiriamali. 
Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) akizungumza katika kikao hicho ambapo  aliihakikishia kamati hiyo kuwa,wizara itakwenda kushughulika maoni waliyoyatoa katika kuboresha na kutunisha Mfuko wa NEDF. (Picha na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara).

Naye, Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) aliihakikishia Kamati hiyo kuwa Wizara itayafanyia kazi maoni na mapendekezo yaliyotolewa ili kuhakikisha SIDO inawezeshwa na inaongezewa mtaji katika Mfuko wa NEDF ili kuongeza kasi ya uanzishaji na ukuzaji wa viwanda vidogo nchini ambavyo vitaongeza ajira na kukuza biashara na uchumi wa nchi. 
Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe akitoa ufafanuzi wa umuhimu wa kutafuta njia mbadala za kutunisha Mfuko wa NEDF kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira wakati wa utoaji wa taarifa ya utekelezaji wa mfuko huo, Februari 5, 2022 katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.(Picha na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara).

Naye, Naibu Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe alisema ni muhimu kuiwezesha SIDO kuongeza mtaji katika Mfuko huo wa NEDF kwa kutumia vyanzo mbalimbali vya fedha ikiwemo kushirikiana na taasisi za umma ili mfuko huo uweze kusaidia wananchi wengi wanaohitaji mitaji ya kuanzisha viwanda vidogo vya kuzalisha bidhaa mbalimbali. 

Awali, akitoa utoaji wa taarifa ya utekelezaji wa Mfuko wa NEDF, Mkurugenzi Mkuu wa SIDO, Mhandisi Prof. Sylvester Mpanduji alieleza kuwa, mfuko huo umeweza kudumu tangu kuanzishwa kwake mwaka 1994 na umepokea jumla ya Shilingi 6,648,886,000 katika kipindi cha mwaka 1994/1995 hadi 2020/2021 kama mtaji na kuukuza hadi kufikia Shilingi 9,765,670,054. 
Mkurugenzi Mkuu wa SIDO, Mhandisi Prof. Sylvester Mpanduji akitoa taarifa ya utekelezaji wa Mfuko wa NEDF kwa Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Viwanda, Biashara na Mazingira, Februari 5, 2022 katika ukumbi wa Bunge jijini Dodoma.(Picha na Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara).

Aidha, Prof. Mpanduji amesema huduma za kifedha za Mfuko wa NEDF zimeendelea kutolewa katika mikoa yote na inajipanga kutoa huduma hiyo katika kila wilaya huku ikitafuta njia bora za kuimarisha mfuko na kukusanya madeni sugu ya mikopo iliyotolewa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news