NAIBU WAZIRI KASEKENYA AKAGUA DARAJA LA BUBUTOLE WILAYANI CHEMBA


Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Godfrey Kasekenya (kulia) akitoa maelekezo kwa Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Dodoma, Mhandisi John Temu, wakati alipokuwa akikagua Daraja la chuma la Bubutole lenye urefu wa mita 60 lililofungwa na wakala ili kufungua mawasiliano ya barabara ya Zamahero – Kinyamshindo (km 124.6), wilayani Chemba mkoani Dodoma.(PICHA NA WUU).
Muonekano wa Daraja la chuma la Bubutole lenye urefu wa mita 60 lililofungwa na Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), wilayani Chemba mkoani Dodoma.
Kazi za utoaji wa mawe chini ya Daraja la chuma la Bubutole lenye urefu wa mita 60 ili kuruhusu maji kupita vizuri na kwa wingi zikiendelea wilayani Chemba, mkoani Dodoma. Daraja hilo la chuma limefungwa na Wakala wa Barabara (TANROADS) mara baada ya daraja la zamani kukatika kutokana ongezeko la maji mengi yaliyotokana na mvua zinazoendelea kunyesha maeneo hayo na Mkoa wa Manyara.
Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Dodoma, Mhandisi John Temu, akifafanua jambo kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Godfrey Kasekenya, wakati akikagua kazi iliyofanywa na wakala ya ufungaji wa Daraja la Chuma mara baada ya daraja la zamani la Mto Bubu kukatika na kusimamisha shughuli za usafirishaji katika Wilaya ya Chemba mkoani Dodoma.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Godfrey Kasekenya (kulia), akiongozana na Kaimu Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Dodoma, Mhandisi John Temu wakikagua Daraja la chuma la Bubutole lenye urefu wa mita 60 lililofungwa na Wakala huo, mara baada ya daraja la zamani kukatika na kufunga mawasiliano ya barabara inayoanzia Zamahero – Kinyamshindo (km 124.6), katika Wilaya ya Chemba, mkoani Dodoma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news