Orodha ya majina ya vijana 470 waliochaguliwa kujiunga na Idara ya Uhamiaji Tanzania

NA GODFREY NNKO

KAMISHNA Jenerali wa Uhamiaji Tanzania,CGI Dkt. Anna Makakala amewatangazia vijana ambao wamechaguliwa kujiunga na Idara ya Uhamiaji kwa cheo cha Konstebo kuripoti Chuo cha Uhamiaji kilichopo Boma Kichakamiba Wilaya ya Mkinga mkoani Tanga siku ya Februari 19,2022 kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana.

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Februari 12, 2022 na Msemaji Mkuu wa Idara ya Uhamiaji, SI Paul Msele ambayo imefafanua kuwa, wafuatao hapa chini wanapaswa kila mmoja afike na mashuka mawili yenye rangi ya bluu bahari, mto mmoja na foronya mbili za bluu bahari zisizo na maua.

Pia wanapaswa kufika na chandarua cha rangi ya bluu, madaftari makubwa 10, ndoo ya plastiki lita 20, fulana mbili za rangi ya dark bluu zenye shingo ya duara zisizo na mchoro wala picha, viatu vya raba na nguo za michezo (tracksuit, bukta na fulana), viatu vya mvua (rainboot), nguo chache nadhifu na za heshima.

Vitu vingine ni kadi ya bima ya afya au fedha shilingi 50,000 kwa wasio na bima ya afya, shilingi 20,000 ka ajili ya kupima afya, shilingi 60,000 ya kununua godoro na fedha za matumizi binafsi. Gharama za usafiri kutoka nyumbani kwenda Tanga Kichakamiba pia zitagharamiwa na mhusika mwenyewe.

Aidha, kila mmoja anapaswa kufika na vyeti halisi vya elimu, kuzaliwa, JKT/JKU, Kitambulisho cha Taifa (NIDA) pamoja na picha tatu za pasipoti za hivi karibuni. Ifuatayo ni orodha ya majina hayo hapa chini;


Post a Comment

0 Comments