Rais Dkt.Mwinyi afanya uteuzi leo

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amemteua, ndugu Mfamau Lali Mfamau kuwa Afisa Mdhamini katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo,Pemba.

Hayo yamebainishwa kupitia taarifa iliyotolewa leo Februari 16, 2022 na Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Zanzibar, Mhandisi Zena A.Said.

Kabla ya uteuzi huo ambao unaanza leo, ndugu Mfamau alikuwa Afisa Mwandamizi wa Ofisi ya Rais Ikulu.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi.

Post a Comment

0 Comments