Rais Samia ateua viongozi mbalimbali leo

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo Februari 4, 2022 ameteua viongozi mbalimbali.
Mosi, Mheshimiwa Rais Samia amemteua Mhandisi John Gervas Nzulule kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ndege za Serikali (TGFA).

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu), Jaffar Haniu ambapo ameeleza kuwa, Bw.Zuhule ni Mhandisi Mwandamizi, TGFA.

Pili, Mheshimiwa Rais Samia amemteua Dkt.Selemani Budeba Majige kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Kampuni ya Puma Energy Tanzania Ltd.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Bw.Majige anaendelea kwa kipindi kingine cha miaka mitatu.

Tatu, Mheshimiwa Rais Samia amemtea Bw.Peter Ilomo na Bibi Suzan Mlawi kuwa Wajumbe wa Baraza la Maadili katika Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma kwa kipindi cha miaka mitatu.

Aidha, taarifa hiyo imefafanua kuwa, teuzi zilizofanywa na Mheshimiwa Rais Samia zimeanza Februari 3, 2022.

Post a Comment

0 Comments