Ruvuma wapuliza kipenga anuani za makazi

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

MKUU wa mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge, amezindua uhamasishaji wa operesheni ya uwekaji wa anuani za makazi na postikodi katika mkoa huo.

Baadhi ya wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana Songea waliohudhuria uzinduzi wa operesheni ya anuani za makazi na Postikodi wakimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge jana(hayupo pichani)wakati wa uzinduzi huo.

Akizungumza jana wakati wa uzinduzi huo alisema,uwekaji wa anuani za makazi utarahisisha kupatikana kwa urahisi watu,ofisi au nyumba na baadhi ya wananchi kupata mikopo katika taasisi za fedha.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge akizungumza jana na wananchi,watumishi wa idara na taasisi za Serikali katika mkoa huo wakati wa uzinduzi wa anuani za makazi na Postikodi katika mkoa huo.

Jenerali Ibuge alisema,katika mkoa huo kazi hiyo itatekelezwa na Serikali kwa kushirikiana na wananchi wa eneo husika, ambapo amewaasa wananchi kuwa tayari na kujitokeza kutekeleza mpango huo.

Amewataka,watendaji wa Serikali watakaopewa jukumu la kusimamia na kutekeleza kazi hiyo,kuhamasisha vyema na kuwaelewesha wananchi kuhusu faida za mpango huo.

Kwa mujibu wake, dhamira ya Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ni kuwafikia wananchi kule walipo ili wanapopata matatizo iwe rahisi kuwafikia na kuwapa msaada.
Baadhi ya wakuu wa idara na taasisi mbalimbali za Serikali wakifuatilia uzinduzi wa operesheni ya anuani ya makazi na Postikodi katika mkoa huo katika viwanja vya Benki ya NMB Mjini Songea.

Hivyo, amewaagiza watendaji watakaohusika katika mpango huo wakiwamo Wakuu wa wilaya, kuhakikisha kazi hiyo inakamilika ifikapo tarehe 30 April, kabla ya kuanza utekelezaji wa sensa ya watu na makazi mwezi Agosti mwaka huu.

Katika uzinduzi huo uliofanyika katika Mtaa wa Nmb mjini Songea Mkuu wa mkoa alisema, lengo la mpango huo ni kuhakikisha kila mtaa unakuwa na jina lake na kila nyumba iwe na namba,jambo litakalo rahisisha utendaji kazi wa Serikali hata ndani ya jamii kwenye shughuli mbalimbali za kiuchumi.

Mkuu wa mkoa alisema, jina la mtaa au barabara litakuwa na maana kwa kila mtumiaji ikiwa litajenga hisia ya umilikishwaji umma katika uundaji wake na unapaswa kuchukuliwa kama kipengelele muhimu katika maeneo ya mjini na vijijini.

Alisema, suala la uwekaji wa anuani za makazi litaonyesha kwa vitendo ukuaji wa uchumi katika mkoa huo na Taifa,hivyo kuingia kwenye matumizi ya teknolojia itakayosaidia mgeni yoyote kutafuta na kufika mahali anapokwenda kwa kutumia GPS badala ya kuuliza kwa watu wanaokaa vijiweni.
Katibu Tawala wa mkoa wa Ruvuma Stephen Mashauri Ndaki kushoto,akimueleza jambo Mkuu wa mkoa huo Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge kulia kuhusu zoezi la anuani za makazi na Postikodi katika mkoa huo lililozinduliwa jana katika viwanja vya Benki ya NMB Songea.

Alisema, ili uchumi wetu uweze kukua kwa haraka na kuendelea kuwa jumuishi kama ambavyo sasa tafiti za Kimataifa zinavyoonesha kuwa Tanzania ni kati ya nchi za Afrika zilizo kinara kwa uchumi jumuishi, ni lazima sisi wenyewe makazi na baishara zetu ziweze kufikika kwa urahisi.

Ibuge alisema,ni muhimu kila mmoja ajulikane alipo,hata akihama afahamike alipohamia,badala ya kuhama usiku bila hata mtendaji wa mtaa kujua na kuwataka wananchi kuboresa mazingira ya kukopeshwa na taasisi za fedha kwa urahisi zaidi.

Aidha alisema,hatua hiyo itazidi kuimarisha upunguzaji wa riba za mikopo kwa taasisi za fedha(Benki)badala ya kuendelea na hoja za kuwepo vihatarishi vingi vya uwezekano wa kutoreshwa mikopo kutokana na watu kutofahamika makazi yao.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Jenerali Wilbert Ibuge kulia,akimpa kibao chenye anuani ya makazi MKurugenzi wa Manispaa ya Songea Dkt Frederick Sagamiko wakati wa uzinduzi wa operesheni ya anuani za makazi na Postikodi mkoa wa Ruvuma,
Meneja wa Benki ya NMB Tawi la Songea Daniel Zake kulia,akipokea kibao kinachoonesha anuani ya makazi wakati wa zoezi la anuani ya makazi na Postikodi katika mkoa huo.

Awali Katibu Tawala wa mkoa huo Stephen Ndaki alisema, uwekaji wa anuani za makazi utarahisisha zoezi la Sensa ya watu na makazi inayotarajia kufanyika mwaka huu na itaonesha maendeleo halisi kwa kutumia mfumo wa kompyuta.

Naye Kamishina wa Ardhi mkoa wa Ruvuma Ildefonce Ndemela alitaja faida za mpango huo ni kuuwezesha mfumo wa anuani za makazi na Postikodi kutumia taarifa za ramani za upimaji na ramani za anga(google map)ambapo kila kiwanja kitakuwa na majina na kufahamika kilipo.

Alisema,kufahamika kwa majina ya nukta ya kiwanja husika,kutamrahisishia mtumiaji wa anuania za makazi na Postikodi kukitambua kiwanja hicho na kumwezesha kufika kwa urahisi kwenye kiwanja na nyumba husika.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news