Tanzania mwenyeji wa Maadhimisho ya 16 ya Siku ya Bonde la Mto Nile

NA PIUS NTIGA

TANZANIA inatarajia kuwa mwenyeji wa maadhimisho ya 16 ya Siku ya Bonde la Mto Nile, ambapo zaidi ya nchi 10 zitashiriki katika maadhimisho hayo.

Nchi hizo ambazo ni washirika wa Bonde la Mto Nile ni pamoja na Tanzania, Burundi, Ethiopia, Kenya, DRC Congo, Misri, Rwanda, Sudan, Sudan Kusini na Uganda.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga amesema maadhimisho hayo yatakayofanyika Jumanne ijayo jijini Dar es Salaam, mgeni rasmi anatarajia kuwa Makamu wa Rais, Dokta Philip Mpango.

Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Tanzania kuwa mwenyeji wa maadhimisho hayo ya Siku ya Bonde la Mto Nile, ambapo mara ya kwanza ilikuwa mwaka 2017.

Aidha, maadhimisho ya mwaka huu pia yanatarajiwa kuwa na washiriki takribani 1,500 kutoka nchi mbalimbali duniani wakiwemo Mawaziri, Mabalozi na wadau wa maendeleo.

Mto Nile wenye urefu wa kilomita 6,695 chanzo chake ni Ziwa Victoria, na ni mrefu kuliko mito yote Duniani.

Unatajwa kuwa ni kichocheo cha uchumi wa nchi za Bonde la Mto Nile kupitia matumizi ya maji majumbai, viwandani, kilimo cha umwagiliaji, mifugo, uvuvi, utalii, mistu, uzalishaji umeme, usafirishaji na shughuli nyinginezo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mpito wa ushirikiano wa Bonde la Mto Nile Mhandisi, Sylvester Matemu ametaja pia faida za bonde hilo la Mto Nile ni uzalishaji wa megawati 80 katika mradi wa Rusumo ambapo ukimalizika nchi za Tanzania, Burundi na Rwanda zitagawana megawati hizo kila nchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news