TARURA kuzaliwa upya, Bashungwa aweka wazi mikakati

NA NTEGHENJWA HOSSEAH-OR TAMISEMI

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa amesema kuanzia mwaka huu Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) watatoa zabuni za ujenzi wa barabara mwezi Aprili, kabla ya mwanka mpya wa fedha kuanza ili kwenda na kasi na kuwahi msimu wa mvua kuanza.
Mhe. Bashungwa ameyasena hayo leo Februari 4, 2022 mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan aliposimama kusalimia wananchi wa Lamadi mkoani Simuyu akielekezea namna ambavyo ameanza kutatua changamoto za wakala huyo.

Amesema, "Mheshimiwa Rais uliponiteua ulinielekeza kubainisha changamoto zainazoifanya TARURA isitoe huduma bora za barabara vijijini, nimezibaini na nimeanza kuzishughulikia na katika kuboresha eneo hilo nimeagiza utaratibu wa kutangaza zabuni za ujenzi wa barabara uanze mwezi Aprili kabla ya mwaka wa fedha mpya kuanza, kama wanavyofanya wenzetu wa TANROADS ili mwaka wa fedha unapoanza Julai Mosi wanakamilisha utaratibu wa kupata wakandarasi na kazi inaanza moja kwa moja.

"Hii itasaidia wakandarasi hao kuwahi 'site' na kuepukana na wakandarasi kufanya kazi msimu wa mvua na kuleta kero zaidi kwa wananchi,"amesema Waziri Bashungwa.

Pia amesema, jambo hilo wameshaliwekea utaratibu na kuanzia mwaka huu ataona ufanisi mkubwa katika utendaji wa TARURA katika kuboresha barabara za vijijini na mijini.

Post a Comment

0 Comments