TASAF yarejesha tabasamu kaya maskini Bagamoyo

NA MWANDISHI MAALUM

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Bagamoyo mkoani Pwani, Shauri Selenda amesema miradi ya TASAF na juhudi za halmashauri kuwawezesha wananchi zimepunguza kwa kiwango kikubwa hali ya umaskini wilayani Bagamoyo ikilinganishwa na miaka ya nyuma.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo, Shauri Selenda akizungumza na wadau wa maendeleo wakati wa ziara ya wadau wa maendeleo ya jamii na maafisa wa mfuko wa jamii TASAF.

Shauri Seleda ameyasema hayo leo wakati Maofisa wa TASAF na ubalozi wa Sweden walipotembelea katika halmashauri hiyo ili kujionea miradi inayotekelezwa na walengwa kutoka kaya masikini wilayani humo.

Amesema kwa sehemu kubwa wanaopewa mikopo na halmashauri ni wale ambao tayari wamenufaika na miradi mbalimbali ya TASAF na wanajua namna ya kuendesha ujasiriamali mbalimbali. 
Mkurugenzi wa Programu za Jamii wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), John Elisha akiangalia bidhaa zilizozotengenezwa kwa mikono na wanufaika wa TASAF wakati walipofanya ziara na wadau wa maendeleo kutoka ubalozi wa Sweden na Ireland. Wengine pichani ni wadau wa maendeleo kutoka Ubalozi wa Sweden na Ireland.

“Tunawapa mafunzo kwanza na hilo limesaidia sana maana wengi tunaowapata ni wanawake na kwa kawaida Pwani hawa ndiyo wanaotunza familia,” amesema Selenda.  

Mmoja wa wanufaika wa TASAF, Zena Hassan amesema uwezeshaji alioupata kutoka TASAF umemuwezesha kusomesha watoto wake wanne na kujenga nyumba yenye thamani ya Shilingi milioni nane katika kipindi cha miaka mitatu. 
Mkurugenzi wa Programu za Jamii wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), John Elisha akiteta jambo na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo, Shauri Selenda (katikati), pamoja na Meneja wa pPogram ya Maendeleo Jumuishi ya Kiuchumi kutoka Ubalozi wa Sweden, Annie Sturinge (kulia), wakati wa ziara ya wadau wa maendeleo na maafisa wa TASAF.

“Kwa namna ambavyo nimenufaika na kujengwa kiujasiriamali sasa naweza kusimama mwenyewe hata utakapofikia muda wa kuondolewa kwenye orodha ya wanufaika,”amesema Zena.

Naye Mkurugenzi wa Programu za Jamii za TASAF, John Elisha amesema TASAF hivi sasa inatekeleza mradi wa kuwajengea uwezo wananchi kiujasiriamali ili kuwaondoa katika umasikini, mradi huo wa mabilioni ya shilingi ulianza mwaka 2020. 
Meneja Uchumi Shirikishi kutoka Ubalozi wa Ireland Eric Masinda akiuliza swali wakati wa ziara ya wadau wa maendeleo ya jamii na maafisa wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), walipotembelea ofisini kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Bagamoyo kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali.

Meneja wa Programu ya Maendeleo Jumuishi ya Kiuchumi kutoka Ubalozi wa Sweden, Annie Sturinge amesema maendeleo ya watu ni jambo muhimu kwa taifa lolote lile.

“Maeneo mengi tunayoenda huwa tunatamani kuona wanufaika wa TASAF wawe wanachangamkia fursa nyingine za mikopo na hilo limefanyika Bagamoyo,”amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news