Utabiri wa hali ya hewa leo, TMA inatoa angalizo la mvua kubwa

Utabiri wa hali ya hewa wa saa 24 zijazo kuanzia saa 3:00 usiku leo Februari 18, 2022 unawasilishwa na mchambuzi Noel Mlay kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).

MATARAJIO YA MVUA KUBWA

>Jumamosi 19/2/2022 

ANGALIZO la mvua kubwa limetolewa kwa maeneo machache ya mikoa ya Dodoma na Morogoro..  

Kwa mujibu wa TMA, athari zinazoweza kujitokeza ni baadhi ya makazi kujaa maji, pamoja na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi. Tafadhali zingatia na ujiandae.
 
>Jumapili 20/2/2022 na Jumatatu 21/2/2022 hakuna tahadhari
 
>Jumanne 22/2/2022

ANGALIZO la mvua kubwa limetolewa kwa maeneo machache ya mikoa ya Iringa, Njombe, Morogoro, Dodoma, Ruvuma, Lindi na Mtwara.
 
Kwa mujibu wa TMA, athari zinazoweza kujitokeza baadhi ya makazi kujaa maji, pamoja na kuathirika kwa baadhi ya shughuli za kiuchumi. Tafadhali zingatia na ujiandae.
Utabiri huu wa hali ya hewa umetolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).

Post a Comment

0 Comments