Viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni leo Februari 11, 2022

NA GODFREY NNKO

LEO Februari 11,2022 kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Randi ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 151.19 na kuuzwa kwa shilingi 152.62 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 20.14 na kuuzwa kwa shilingi 20.30.
Kwa upande wa Franka ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.18 na kuuzwa kwa shilingi 2.24 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.623 na kuuzwa kwa shilingi 0.65.

Aidha, kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania, Franka ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.206.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya BoT,dola ya Marekani nchini inabadilishwa kwa Shilingi 2286.723 huku ikiuzwa kwa Shilingi 2309.6 na Paundi ya Uingereza inabadilishwa kwa Shilingi 3102.85 huku ikiuzwa kwa Shilingi 3135.5.

Kwa mujibu wa BoT, Euro ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi 2614.87 na kuuzwa kwa shilingi 2641.25.

Wakati huo huo,Yuan ya China inanunuliwa kwa shilingi 359.72 huku ikiuzwa kwa shilingi 363.246 huku Yen ya Japan ikinunuliwa kwa shilingi 19.75 na kuuzwa kwa shilingi 19.95.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news