Viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni leo Februari 15,2022

NA GODFREY NNKO

LEO Yuan ya China inanunuliwa kwa shilingi 359.87 huku ikiuzwa kwa shilingi 363.1 na Yen ya Japan inanunuliwa kwa shilingi 19.82 na kuuzwa kwa shilingi 20.014.

Randi ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 151.4 na kuuzwa kwa shilingi 152.824 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 20.14 na kuuzwa kwa shilingi 20.303.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Februari 15, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania.

Kwa upande wa Franka ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.18 na kuuzwa kwa shilingi 2.24 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.62 na kuuzwa kwa shilingi 0.67.

Aidha, kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania, Franka ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.206.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya BoT,dola ya Marekani nchini inabadilishwa kwa Shilingi 2286.713 huku ikiuzwa kwa Shilingi 2309.6.
Paundi ya Uingereza inabadilishwa kwa Shilingi 3095.752 huku ikiuzwa kwa Shilingi 3127.2 wakati Euro ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi 2592.7 na kuuzwa kwa shilingi 2618.833.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news