Viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni leo Februari 21, 2022

NA GODFREY NNKO

LEO Februari 21,2022 kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Randi ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 152.23 na kuuzwa kwa shilingi 153.8 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 20.13 na kuuzwa kwa shilingi 20.295.
Kwa upande wa Franka ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.18 na kuuzwa kwa shilingi 2.24 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.63 na kuuzwa kwa shilingi 0.66.

Aidha, kwa mujibu wa Benki Kuu ya Tanzania, Franka ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya BoT,dola ya Marekani nchini inabadilishwa kwa Shilingi 2286.8 huku ikiuzwa kwa Shilingi 2309.63.

Paundi ya Uingereza inabadilishwa kwa Shilingi 3114.8 huku ikiuzwa kwa Shilingi 3146.9.
Kwa mujibu wa BoT, Euro ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi 2598.8 na kuuzwa kwa shilingi 2625.125.

Wakati huo huo,Yuan ya China inanunuliwa kwa shilingi 361.641 huku ikiuzwa kwa shilingi 364.8 huku Yen ya Japan ikinunuliwa kwa shilingi 19.9 na kuuzwa kwa shilingi 20.6

Post a Comment

0 Comments