Watumishi wa Maliasili na Utalii wapewa maelekezo muhimu

NA HAPPINESS SHAYO-WMU

NAIBU Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja amewataka watumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii wawe mstari wa mbele katika kuhamasisha na kutangaza utalii ili kuvutia watalii wengi zaidi kwenda kutembelea vivutio vilivyopo hapa nchini.
Mhe. Mary ameyasema hayo leo Februari 15,2022 jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na watumishi wa wizara hiyo na taasisi zake ambapo amesema kuwa iwapo kila mtumishi ataamua kutumia nafasi yake kutangaza utalii mwamko wa Watanzania kutembelea vivutio vilivyopo utaongezeka.

"Tunatakiwa sisi wenyewe tuoneshe mfano kwa kutafuta masoko na kuhamasisha Utalii, kutafuta mikutano mbalimbali inayo fanyika maeneo ije kufanyika Tanzania tuuze huduma za kumbi zetu za Kimataifa, bidhaa na bidhaa zetu kupitia hiyo mikutano,"amesema Mhe.Masanja.
Amesema kuwa, kupitia kuuza fursa hizo na mazao mbalimbali ya utalii yaliyopo hapa nchini hususani mikutano ya Kimataifa itakuwa kichocheo kwa watalii wengi kuhamasika kufika kwenye vivutio vilivyopo.

Mhe. Mary Masanja amesisitiza kuwa ni wajibu wa kila wizara na taasisi kutangaza utalii hatua itakayosaidia kuongeza Pato la Taifa kupitia watalii wanaokuja kutembelea vivutio hivyo hapa nchini.

Aidha, katika hatua nyingine Naibu Waziri Mhe. Mary Masanja ametoa wito kwa Wanawake wote wa Wizara hiyo kuyatumia Maadhimisho yajayo ya Siku ya Wanawake Duniani yatakayoadhimishwa Machi 8 mwaka huu kupaza sauti zao kwa kuhamasishana kutangaza Utalii wa ndani na kutembelea vivutio vilivyopo.
‘’Sasa hivi tumekuwa na matukio ya watu kujiua, tunataka tupunguze tatizo hili kwa kufurahi kukutana pamoja ,kubadilisha mawazo.Tunataka kuanzia tarehe 1 mpaka 8 mwezi Machi mwaka huu sisi wenyewe tuutangaze utalii wetu,"amesisitiza.

Katika hatua nyingine, Mary amewataka watumishi hao kufanya kazi kwa uadilifu na upendo na kuepuka mambo yayorudisha nyuma utendaji wao mahali pa kazi huku akiwahimiza kuendelea kufanya kazi kwa ushirkiano ili Sekta ya Utalii izidi kusonga mbele.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news