Waziri Dkt.Mwigulu ateua wajumbe saba wa Bodi ya Chuo cha EASTC

NA GODFREY NNKO

WAZIRI wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt.Mwigulu Lameck Nchemba (Mb) ameteua wajumbe saba wa Bodi ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC).

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa umma na Mkuu wa Kitengo cha Mwasiliano Serikali kupitia Wizara ya Fedha na Mipango, Bw.Benny Mwaipaja.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi huo unakuja kufuatia uteuzi uliofanywa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kumteua Profesa Ahmed Mohame Ame kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika.

Wajumbe walioteuliwa na Mheshimiwa Waziri Dkt.Nchemba ni Dkt.Emmanuel Msovu Sadiki, Bw.Juma Hassan Reli, Bi.Nyambilila Mbonile Minga.

Wengine ni Bw.Joachim Clemence Otaru, Bw.Omary Waziri Khama, Dkt.Amina Suleiman Msengwa na Bw.Omari Iddi Abdallah.

Aidha, kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kupitia Wizara ya Fedha na Mipango, uteuzi wa wajumbe hao umeanza Februari Mosi, 2022.
Waziri wa Fedha na Mipango, Mheshimiwa Dkt.Mwigulu Lameck Nchemba (Mb).

Post a Comment

0 Comments