Waziri Dkt.Ndumbaro aongoza zoezi la uvishaji vyeo viongozi wa TANAPA, NCAA

NA MWANDISHI MAALUM

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dkt. Damas Ndumbaro leo  Februari 18, 2022 ameongoza zoezi la uvishaji vyeo kwa viongozi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) na Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA).

Viongozi waliovishwa vyeo hivyo ni William Mwakilema ambaye hivi karibuni aliteiliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwa Kamishna wa Uhifadhi wa Hifadhi za Taifa (TANAPA).

Viongozi wengine waliovishwa vyeo ni kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro (NCAA) ambao ni Bw. Needpeace Wambuya aliyepandishwa cheo kuwa Naibu kamishna wa Uhifadhi (Huduma za Shirika) na Bw. Elibariki Bajuta aliyepandishwa cheo kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi (Huduma za Ulinzi).

Post a Comment

0 Comments