Waziri Mkuu atoa muongozo kwa wakazi wa Loliondo

NA MWANDISHI MAALUM

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali inaangalia utaratibu utakaofaa kuhusu suala la uhifadhi katika eneo la Loliondo lililopo kwenye wilaya ya Ngorongoro mkoani Arusha.

"Katika mjadala wetu wa leo, mmetoa maoni nasi tumeyapokea. Bado Serikali inayaangalia maslahi mapana ya umma. Tutawashirikisha pia ni lipi lina maslahi mapana kwa Watanzania."
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akislimiana na viongozi wakati alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa Waso, Loliondo wilayani Ngorongoro.

Ametoa kauli hiyo Februari 14, 2022 wakati akizungumza na wadau wa uhifadhi kwenye kikao kilichofanyika Wasso-Loliondo. Amesema Serikali imepokea maoni waliyoyatoa, yatayojumuishwa na kuyawasilishwa kwa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Pia, Mheshimiwa Majaliwa amesema alichoenda kufanya leo ni utekelezaji wa ushauri uliotolewa na wabunge kwa Serikali kupitia Mwenyekiti wa Kamati wa Maliasili na Utalii iliyoielekeza Serikali iende katika maeneo ya Loliondo, Ngorongoro na Sale na kuzungumza na wananchi.  Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza na wadau wa Uhifadhi, katika kikao kilichofanyika viwanja vya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Waso, Loliondo wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha.

“Kama ambavyo Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan ameagiza lazima tuimarishe utalii na kuhakikisha wananchi wanashirikishwa, Waheshimiwa wabunge ambao ndio wawakilishi wametoa maoni yao ikiwemo kushauri suala la ushirikishwaji na ndio maana leo nimekuja hapa kuwasikiliza”.

Waziri Mkuu amesema wote tunatambua kuwa idadi ya watu na mifugo imeongezeka ndani ya hifadhi ambapo tusipotafuta suluhisho la kudumu hifadhi zetu zitaathirika. “Sisi sote tunatambua eneo hili ni la utalii, lazima tufike mahali tuamue kama tunataka utalii au la," amesema.  Baadhi ya wakazi wa Waso, Loliondo wilayani Ngorongoro na wadau wa uhifadhi wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa wakati alipozungumza nao, Februari 14, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Waziri Mkuu amesema amefarijika kusikia kwamba wachangiaji wote waliozungumza hakuna aliyesema ardhi ni yao. "Kati ya mambo yamenifariji, sijasikia mtu akisema ardhi yetu, ardhi yetu. Sote tunatambua kuwa ardhi iliyo ndani ya mipaka ya nchi hii ni ya umma lakini tumeikasimu kwa Mheshimiwa Rais kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania."

Katika kikao hicho, wananchi wa makundi mbalimbali walipewa nafasi kutoa maoni yao wakiwemo mbunge, madiwani, malaigwanan, wanamije (batemi) na wenyeviti wa vijiji. Katika maoni yao, wengi wao walisema wako tayari kushirikiana na Serikali kuendelea kutunza rasilimali za Taifa.

Waliomba wapatiwe elimu ya uzazi wa mpango, wapimiwe ardhi za vijiji ili kupunguza migogoro inayojitokeza mara kwa mara. Wilaya ya Ngorongoro ina tarafa tatu za Loliondo, Sale na Ngorongoro.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news