Wizara yatoa maelekezo kwa makamanda wa Jeshi la Polisi nchini

NA MWANDISHI MAALUM

NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amewaagiza Makamanda wa Jeshi la Polisi nchini kutumia wataalamu wao hadi wa ngazi ya tarafa kudhibiti vitendo vya uhalifu vinavyotokea nchini.
Amesema kwamba haiwezekani Jeshi la Polisi kumwachia Rais Samia Suluhu Hassan kuzungumzia jambo ambalo Makamanda wa Polisi wapo na wana uwezo wa kulisimamia kwenye maeneo yao.
“Niwaombe Makamanda wa Polisi Mikoa yote, tumieni wataalamu mlio nao kudhibiti vitendo vya uhalifu vinavyotokea nchini. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhadisi Hamad Masauni na mimi, haturidhishwi kabisa kumwachia Mheshimiwa Rais kuzungumzia jambo ambalo mpo na mna uwezo wa kulisimamia;

Naibu Waziri Sagini amesema hayo Februari 7,2022 mbele ya mamia ya wananchi wa Bunda, baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika Viwanja vya Sabasaba vilivyopo Shule ya Msingi Miembeni, Wilaya ya Bunda Mjini mkoani Mara.
Aidha, akizungumza na wananchi hao amewataka kuwa raia wema na kuepuka vitendo vya kiuhalifu kwa sababu Jeshi la Polisi halitawafumbia macho wahalifu. Amesema Jeshi hilo linawataalamu wa Upelelezi, wataalamu wa Jinai kwahiyo wahalifu wote watashughulikiwa.

“Mheshimiwa Rais kwa siku za hivi karibuni kumeibuka matukio ya ovyo yanayodhalilisha utu wetu kwa baadhi ya watu kuwaua wenzao. Jambo hili halikubaliki. Ni aibu kuwa na taifa la watu wanachinjana tena wengine ndugu kwa ndugu na wengine wakwe, ni fedheha ambayo haiwezi kuvumilika”.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini akizungumza na wananchi wa Bunda, baada ya kupewa nafasi ya kuongea na Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika Viwanja vya Sabasaba Miembeni, Wilaya ya Bunda,Mara.Amewataka kuwa raia wema kwa kuepuka vitendo vya kiuhalifu.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Jumanne Sagini amewaagiza Makamanda wa Jeshi la Polisi Mikoani kutumia wataalumu wao hadi wa ngazi ya tarafa kudhibiti matukio ya mauaji yanayotokea nchini.Amesema hayo kwenye Mkutano wa Hadhara uliofanyika, Wilaya ya Bunda  Mkoa wa Mara.
Pia Naibu Waziri Sagini amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu ujenzi wa Ofisi za Makamanda wa Polisi nchini. Amesema ujenzi huo utaimarisha mazingira ya kazi ili wataalamu waweze kufanya kazi zao vizuri.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news