Azam FC kukutana na DTB kesho

NA MWANDISHI WETU

TIMU ya Azam FC kesho itakuwa na mechi ya kirafiki dhidi ya DTB katika dimba la Azam Complex lililopo Kata ya Chamazi Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Azam kupitia mechi hiyo ni sehemu ya maandalizi ya mchezo ujao wa Ligi Kuu ya NBC ya Tanzania Bara dhidi ya Yanga SC Aprili 6,2022.

Mtanage huo ambao unatarajiwa kuwa wa kuvutia baina ya Wanajangwani ambao wapo kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu ya NBC utapigwa katika dimba la Azam Complex lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam

Aidha, kwa DTB mechi hiyo ni ya kujipanga kwa michezo yake ijayo ya ligi ya kuwania kupanda Ligi Kuu, ijulikanayo kama Championship.

Pia Yanga SC watakuwa na mechi ya kujipima dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar itakayopigwa katika dimba la Azam Complex.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news