BASATA kutuliza joto Shirikisho la Muziki Tanzania (SMT) kuhusu Msemaji

NA MWANDISHI WETU

BAADA ya kuonekana hali ya kutoelewana miongoni mwa wasanii wa muziki kuhusu uteuzi wa Steve Nyerere kuwa Msemaji wa Shirikisho la Muziki Tanzania (SMT), Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) limesema pande zote mbili zina hoja na hivi karibuni watalitolea majibu.
BASATA limebainisha hayo kupitia taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo Machi 23, 2022 na Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA, Matiko Mniko muda mfupi baada ya kumaliza kikao na viongozi hao kilichoketi kwa saa tano.

Mniko amesema kuwa, waliziita pande zote mbili za uongozi na wakawasikiliza na kugundua kila upande una hoja na BASATA watatoa uamuzi wa jambo hilo hivi karibuni.

"Moja ya majukumu tuliyopewa BASATA ni kushughulikia pia migogoro inapotokea kwa wasanii nasi tulichofanya leo ni moja ya jukumu hilo kwa kuwaita na kuwasikiliza kila upande na hoja zao,"amesema Mniko.

Amesema kuwa, baada ya kumaliza kupitia hoja zao baraza hilo litatoa majibu mapema iwezekanavyo katika kumaliza mgogoro huo.

"Lengo sio kuona wasanii wanafarakana bali tunataka wafanye kazi kwa kushirikiana na kuipeleka sanaa mbele," amesisitiza Katibu huyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news