Doreen:Mzee Mrema ninamrudisha ujanani, ninyi wenye mmeona leo alivyo

*Asema si mwanamke wa kupewa, amesimama mwenyewe na hata mali anazo

NA MWANDISHI WETU

MWENYEKITI wa Chama cha TLP, Augustino Lyatonga Mrema amefunga ndoa na Doreen Kimbi.

Ndoa hiyo imefungwa leo Machi 24,2022 katika Kanisa Katoliki Parokia ya Uwomboni Kiraracha mkoani Kilimanjaro.

Baada ya kufungwa ndoa hiyo, mke wa Mzee Mrema, Doreen mesema kuwa atamrudisha mzee Mrema ujanani.
"Mpaka kufikia hivi alivyo nimemfanya hivyo katika kipindi cha uchumba, nimemweka kuwa sawa, vitu vyote anavyohitaji anavipata.

"Kwa sasa amebadilika, nimeamua mwenyewe na sijashurutishwa na mtu na watarajie kuona anapendeza, nataka hadi awe kijana," amesema Doreen.
Pia ameongeza kuwa, hajafuata mali kwa mzee Mrema.

"Mimi si mwanamke wa kupewa, nimesimama mwenyewe na hata mali ninazo. Nilianza kujitafutia mimi, siendi kwake (Mrema) kutafuta mali. Lakini nikimlea vizuri akanipa mali si vibaya, kwani ni mke wake,"amesema Doreen

Mrema ambaye aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali serikalini, kuwa mbunge na kugombea urais wa Tanzania, Machi 21,2022 wakati akizungumza na waandishi wa habari nyumbani kwake katika Kijiji cha Kiraracha alisema, amefikia hatua hiyo baada ya mke wake kufariki mwaka jana.

Alisema alibaki mpweke na kutokana na hali yake ya kiafya akaona ni vyema kumtafuta mwenza ambaye atamhudumia na kumtunza na alipata baraka zote za familia pamoja na kanisa.

Post a Comment

0 Comments