Maandalizi ufunguzi wa Daraja la Tanzanite kesho yafikia asilimia 95

NA MWANDISHI MAALUM

MAANDALIZI ya eneo litakalotumiwa kwa ajili ya hafla ya uzinduzi wa daraja la Tanzanite linalokatisha baharini eneo la Sea View Upanga kuelekea Oysterbay jijini Dar es Salaam ambalo kesho Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kulifungua yamekamilika kwa asilimia 95.
Mkuu wa Itifaki Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Yusuf Mndolwa Tindi kulia akizungumza na Bw. Gibson Mwaya Afisa Sayansi ya Jamii Mkuu Wakala wa Barabara (TANROADS) katikati mara baada ya kukagua maandalizi ya eneo litakalotumiwa kwa ajili ya hafla ya uzinduzi wa daraja la Tanzanite ilnalokatisha baharini eneo la Sea View Upanga kuelekea Oysterbay jijini Dar es Salaam, ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuweka historia nyingine kwa kulifugua rasmi daraja hilo lenye urefu wa kilomita 1.03 pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa kilomita 5.2. (Picha zote na Fullshangwe Blog).

Kesho, Mheshimiwa Rais Samia atalifugua rasmi daraja hilo lenye urefu wa kilomita 1.03 pamoja na barabara unganishi zenye urefu wa kilomita 5.2.

Bw. Gibson Mwaya ambaye ni Afisa Sayansi ya Jamii Mkuu Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) amesema kila kitu kinakwenda sawa na maandalizi yamekamilika kwa kiasi kikubwa.

Mwaya ameongeza kuwa, Rais Samia Suluhu Hassan anakwenda kuandika historia kwa watanzania kwa kufungua rasmi daraja hilo ambalo lilianza kujengwa mwaka 2018 baada ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Awamu ya Tano Hayati Dkt. John Pombe Magufuli kuweka jiwe la msingi kwa ajili ya kuanza kwa ujenzi huo.
Bw. Gibson Mwaya ambaye ni Afisa Sayansi ya Jamii Mkuu Wakala wa Barabara (TANROADS) kulia akimsikiliza Mhandisi Mwanaisha Rajabu ambaye ni Mhandisi Miradi wa Mkoa wa Dar es Salaam TANROADS wakati wakijadiliana jambo katika maandalizi hayo.
Baadhi ya maofisa kutoka Wilzara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wakijadiliana jambo wakati wakiwa katika shughuli nzima ya maandalizi ya uzinduzi wa daraja hilo.
Bw. Gibson Mwaya Afisa Sayansi ya Jamii Mkuu Wakala wa Barabara (TANROADS) kulia akielekeza jambo wakati wa maandalizi hayo.
Picha mbalimbali zikionesha maeneo na majukwaa mbalimbali yakiendelea kupambwa na kuwekwa sawa kwa ajili ya uzinduzi wa Daraja la Tanzanite ambalo kesho Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kulifungua rasmi.
Amesema kwamba, sherehe hiyo itakuwa ni kubwa na itakuwa ni fursa kwa watanzania kuona yale yaliyoahidiwa na serikali yao kuwa yametekelezwa ambapo tayari wameruhusu magari yaanze kupita toka mwezi wa pili mwaka huu.

Bw. Mwaya amewakaribisha wananchi wa mkoa Dar es Salaam na maeneo mbalimbali nchini kufuatilia kwenye vyombo mbalimbali vya habari ili kujionea tukio hilo moja kwa moja kupitia runinga na mitandao ya kijamii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news