Makamishna Wasaidizi wa Uhifadhi TANAPA wavishwa vyeo

NA MWANDISHI WETU

KAMISHNA wa Uhifadhi wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), William Mwakilema amewavisha vyeo Makamishna Wasaidizi wa Uhifadhi waliopandishwa vyeo hivi karibuni.
Tukio hiko limefanyika leo Machi 23, 2022 katika Hifadhi ya Taifa Ziwa Manyara mkoani Manyara.
Waliovalishwa vyeo ni Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi, Fidelis Kapalata na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Moses Nonga ambao kabla ya hapo walikuwa Maafisa Wakuu wa Uhifadhi.

Kamishna Msaidizi Fidelis Kapalata kwa niaba ya mwenzake ameahidi ushirikiano kwa viongozi wenzake wa shirika ili kuweza kufikia malengo tarajiwa ya shirika.Kamishna Mwakilema amewataka makamishna wapya kufanya kazi zao kwa kuzingatia viapo vyao, weledi, bidii na maarifa ili kulifanya shirika lisonge mbele katika majukumu yake ya uhifadhi.

"Ni vema tufanye kazi kama timu moja kwa ushirikiano, tuwe mfano kwa tunaowaongoza pamoja na kuwajengea uwezo wa kushika nafasi za uongozi hapo baadaye,"amesema Kamishna Mwakilema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news