Prof.Mkenda, Balozi wa Qatar nchini waangazia Sekta ya Elimu

NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Adolf Mkenda (Mb) tarehe 24 Machi,2022 amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Qatar nchini, Mhe. Balozi Hussain Ahmad Al Homaid jijini Dar es Salaam.
Viongozi hao pamoja na mambo mengine wamezungumzia ushirikiano wa nchi hizo mbili katika kuimarisha na kuongeza fursa za elimu nchini.
Kikao hicho pia kimehudhuriwa na Mkurugenzi wa Idara ya Mashariki ya Kati, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Hemedi Mgaza.

Post a Comment

0 Comments