Rais Samia azindua nyumba 644 za waliokuwa wakazi wa Magomeni Kota, atoa rai

NA MWANDISHI WETU

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amesema watu waliokuwa wakisema miradi iliyaochwa na mtangulizi wake,Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli haitaendelezwa hawakuwa sahihi kwa sababu Serikali inayoongoza nchi ni ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mheshimiwa Rais Samia ameyasema hayo leo Machi 23, 2022 wakati akizindua nyumba za Magomeni Kota 644 zilizojengwa kwa thamani ya zaidi ya sh.bilioni 51 na Wakala wa Majengo Tanzania (TBA).

Ni kupitia mchakato wa ujenzi huo ambao ulianza 2016 chini ya uongozi wa Rais wa Awamu ya Tano, Hayati Dkt.Magufuli..

“Kulikuwa na maneno mengi, iliyoachwa haitaendelezwa ukiuliza sababu hakuna. Hakukuwa na sababu ya kwamba miradi hiyo isiendelezwe, kwani ilianzishwa na kuagizwa ndani ya Ilani ya CCM.

"Sasa kwa kunitazama sura na kusema isingeweza kutekelezeka miradi, nadhani hekima haikutumika. Wanaposema miradi haitaendelezwa nadhani upeo wao wa kufikiria ni mdogo sana. Hata miradi hii ilivyoanzishwa nilikuwa Makamu wa Rais, kwa hiyo ni sehemu tangu kuanza kwake na kutekelezwa,” amesema Rais Samia wakati akizindua mradi huo.

"Lakini tuwaombee nasi tujiombee kwa Mungu atupe nguvu, uwezo na hekima zaidi ili tuweze kuendeleza miradi kwa maendeleo ya Taifa,"amefafanua Mheshimiwa Rais Samia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news