Tanzania,Liechtenstein zakubaliana kuweka mpango mkakati kuwekeza katika kilimo hai,kuongeza thamani ya mazao mikoa ya Morogogo na Dodoma

*Pia wakubaliana kuangazia maeneo mapya ya ushirikiano katika sekta za Utalii, Viwanda na Elimu

NA MWANDISHI WETU

SERIKALI ya Tanzania na Liechtenstein zimekubaliana kuweka mpango mkakati wa kuwekeza katika kilimo hai na kuongeza thamani ya mazao ya kilimo katika mikoa ya Morogogo na Dodoma.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Liechtenstein, Mhe. Dominique Hasler akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje wa Liechtenstein Mhe. Dominique Hasler ambaye yuko nchi kwa ziara ya kikazi.

Katika mazungumzo hayo viongozi hao wamekubaliana kuangazia maeneo mapya ya ushirikiano katika sekta za Utalii, Viwanda, na Elimu, hususan kumuendeleza mtoto wa kike katika masomo ya sayansi na teknolojia.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula akiongea na Waziri wa Mambo ya Nje wa Liechtenstein, Mhe. Dominique Hasler katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,Balozi Liberata Mulamula akimfafanulia jambo Waziri wa Mambo ya Nje wa Liechtenstein, Mhe. Dominique Hasler katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

“Tumekubaliana mara baada ya ziara yake tuweze kuangazia namna gani tunaweza kudumisha na kuendeleza maeneo mapya ya ushirikiano baina yetu kwa maslahi ya Tanzania na Liechtenstein,”amesema Balozi Mulamula.

Naye Waziri wa Mambo ya Nje wa Liechtenstein,Mhe. Dominique Hasler amesema Liechtenstein ina uhusiano imara na wa siku nyingi, na tumekuwa tukisaidia miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo hapa nchini Tanzania hivyo kuja kwetu hap ani kuja kuiona miradi hiyo na kutuwezesha kujadiliana kwa pamoja ni namna gani tunaweza kuendele kushirikiana katika miradi hiyo.
Kikao cha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula na Waziri wa Mambo ya Nje wa Liechtenstein, Mhe. Dominique Hasler kikiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.
Mjumbe aliyeambatana na Waziri wa Mambo ya Nje wa Liechtenstein, Mhe. Dominique Hasler akifafanua jambo wakati wa kikao.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula katika picha ya pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje wa Liechtenstein, Mhe. Dominique Hasler na Mkurugenzi Idara ya Ulaya na Amerika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Swahiba Mndeme (kulia mwa Balozi Mulamula). Wengine ni Viongozi walioambatana na ujumbe wa Waziri Hasler pamoja na Afisa Mwandamizi kutoka wizarani.

"Katika kikao changu na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania tumejadili mambo mbalimbali ya ushirikiano baina ya nchi zetu, lakini kubwa kabisa tumekubaliana kuongeza maeneo mapya ya ushirikiano," amesema Waziri Hasler.

Waziri Hasler akiwa nchini atatembelea miradi mbalimbali ya kilimo hai inayotekelezwa kwa ushirikiano kati ya Tanzania na Liechtenstein kupitia Sustainable Agriculture Tanzania (SAT) katika mkoa wa Morogoro na Dodoma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news