Ufanisi wa Chuo cha Taifa cha Utalii waigusa Serikali, Katibu Mkuu atoa maelekezo

*Asisitiza umuhimu wa kuwaendeleza watumishi kielimu 

NA HUGHES DUGILO

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt.Francis Michael amekipongeza Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) kwa namna kinavyotekeleza majukumu yake ikiwa ni pamoja na kusimamia mafunzo ya UVIKO-19 chini Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa katika mikoa nane ya Tanzania Bara kwa awamu ya kwanza yaliyokamilika hivi karibuni.
Dkt.Michael ameyasema hayo alipofanya ziara ya kutembelea chuoni hapo na kufanya mazungumzo na watumishi wacChuo hicho kutoka katika Kampasi ya Temeke na Bustani jijini Dar es Salaam.

Amesema kuwa, chuo hicho kimekuwa msaada mkubwa kwa wananchi wanaohitaji kupata ujuzi wa masuala mbalimbali katika Sekta ya Utalii na kwamba chuo kimekuwa kikitekeleza majukumu yake kwa ufanisi mkubwa.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Francis Michael akizungumza na watumishi wa na viongozi wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) alipofanya ziara chuoni hapo Machi 25,2022 kujionea shughuli za chuo hicho na kuzungumza na watumishi ikiwa ni sehemu ya ziara yake aliyoifanya ya kutembelea taasisi zilizopo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii.

Aidha, ameeleza kuwa ziara hiyo pia imelenga kufanya mazungumzo ya pamoja na watumishi wa chuo hicho ili kusikiliza changamoto zao na kupata maoni yao juu ya masuala mbalimbali yakiwemo uboreshwaji wa mazingira ya kazi zao.

"Ndugu zangu leo nimekuja kuwapongeza kwa kazi kubwa mnayofanya, lakini pia kutaka kuwasikiliza tuzungumze pamoja ili kupata maoni na mawazo yenu na kupata ufumbuzi wa changamoto zetu kwa ujumla.

"Hongereni sana mmefanya kazi kubwa sana, mmefanya mambo makubwa nawapongoza kwa kazi kubwa mnayofanya na hali kubwa mlionayo ya kufanya kazi ndio maana ni vizuri watumishi kukutana na viongozi wao kama hivi leo kuzungumza kwa pamoja na kujua shida zao, na mimi nimekuja kuwapongeza, lakini pia kuwasikiliza,"alisema Dkt.Michael.

Ameongeza kuwa, jambo kubwa katika utumishi wa umma ni kuchapa kazi kwa nidhamu ya hali ya juu, kwa weledi na kwa juhudi kubwa, kufuata miongozo na taratibu zilizopo, kutii viongozi sambamba na kutumia muda mwingi kwenye kazi.
Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prisca Rwangila (kushoto) aliyesimama akizungumza katika mkutano huo akimkaribisha mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Francis Michael kuzungumza na watumishi wa Chuo cha NCT. (kulia aliyekaa) ni Mkurugunzi wa Fedha na Utawala wa Chuo hicho, CPA Munguabela Kakulima.
Mkurugunzi wa Fedha na Utawala wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) CPA Munguabela Kakulima akizungumza wakati alipokuwa akifanya utambulisho katika mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Francis Michael (kushoto) akizungumza na Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prisca Rwangila (kulia) wakati wa mkutano huo.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Dkt. Francis Michael (kushoto) na Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT), Dkt. Shogo Mlozi Sedoyeka (kushoto) wakiteta jambo mara baada ya KatikibuMkuu kumaliza kuzunguza na watumishi wa Chuo hicho.
Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii Prisca Rwangila (kushoto) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Chuo cha taifa cha Utalii (NCT) CPA. Munguabela Kakulima mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo Jijini Dar es Salaam.

Amesema, chuo hicho kina bahati ya kuwa na watumishi wengi vijana wanaofanya kazi kwa nidhamu ya hali ya juu hivyo kuutaka uongozi wa chuo hicho kuwatafutia nafasi za masomo watumishi hao ili kujiendeleza na kwamba kwa kufanya hivyo kutaongeza morali ya kazi kwa watumishi hao na kufanyakazi kwa bidii na weledi.

"Hapa naona kuna damu changa, kuna wakufunguzi wengi wadogo nikuombe Mkurugeni kuwatafutia nafasi za masomo wajiendeleze kimasomo, wapelekeni kwenye masomo kwani kusomesha watumishi ni kazi ya taasisi, kuna faida kubwa ikiwemo kumfanya mtumishi aipende taasisi, hivyo nikuombe sana Mkurugenzi tafuta hela na mimi nitakusaidia kutafuta hela ili hawa watumishi waende shule wakirudi utakuwa umeongeza motisha ya kazi na kuendelea kuipenda kazi yao na kuifanya taasisi kuwa na wataalamu wa kutosha na hivyo kufikia malengo yake,"ameongeza Dkt.Michael.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) Dkt. Shogo Mlozi Sedoyeka akizungumza alipokuwa akitoa hotuba yake ya utangulizi katika mkutano huo uliofanyika Machi 25,2022 katika chuo hicho jijini Dar es Salaam.

Awali kitoa hotuba ya utangulizi Afisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT), Dkt.Shogo Mlozi Sedoyeka ameelezea kazi mbalimbali za utoaji mafunzo zinazofanywa na chuo hicho katika kampasi zake nne ikiwemo Bustani iliyokopo katikati ya Jiji la Dar es Salaam, Temeke, Arusha na Mwanza, na kwamba kwa sasa chuo hicho kinaendelea na jitihada zake za kuhakikisha kinapata watumishi wa kutosha kupitia Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ili kukiwezesha chuo kuendelea na mipango yake mbalimbali.

Aidha, amesema kuwa katika mwaka huu wa fedha chuo hicho kimekuwa na vipaumbele saba ambavyo mpaka sasa ndio majukumu yao wanayoendelea kuyatekeleza ikiwa ni pamoja na kuimarisha mafunzo na shughuli za chuo hicho.

"Katika mwaka huu wa fedha tumekuwa na vipaumbele ambavyo ni pamoja na kuimarisha kampasi yetu mpya iliyopo kule Mwanza, kuandaa sheria mpya ya uendeshaji wa chuo, kuongeza wigo wa kukusanya mapato ili kupunguza utegemezi kutoka Serikali Kuu.



Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prisca Rwangila (kushoto) akijadiliana jambo na Mkurugenzi wa Utawala na Fedha wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT), CPA. Munguabela Kakulima mara baada ya kumalizika kwa mkutano huo jijini Dar es Salaam.


"Lakini pia kulikuwa na kipaumbele cha kuongeza uwezo wa kufanya utafiti katika Sekta ya Utalii na Ukarimu, pia tuna lengo la kupanua Kampasi yetu ya Arusha ambapo kimkakati Arusha ndio mkoa unaoongoza katika shughuli za utalii, lengo letu lingine ni kuhamisha kampasi yetu ya Temeke iliyopo Wilaya ya Temeke,"ameeleza Dkt.Sedoyeka.

Pia Dkt.Sedoyeka amemueleza Katibu Mkuu huyo changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo ikiwemo uhaba wa watumishi katika maeneo mbalimbali, changamoto ya chuo kutokuwa na muundo wake, miundombinu chakavu, madeni ya ndani na nje ya muda mrefu,ufinyu wa bajeti ambapo ameeleza kuwa changamoto hiyo imefanyiwa kazi kwa kiasi kikubwa na katika mwaka huu wa fedha chuo kimepata fedha kwa wakati hivyo kuishukuru Serikali na kwamba ana imani kubwa kwa mwaka ujao wa fedha wataongezewa fedha katika bajeti yao.
Katika kikao hicho ambacho Katibu Mkuu aliambatana na Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Prisca Rwangila ambapo watumishi wa chuo hicho walipata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali ambayo Katibu Mkuu, Dkt.Michel aliyatolea ufafanuzi na mengine kuyatolea majibu ya papo kwa hapo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news